Mimi ninawabatiza kwa maji kuonesha kuwa mmebadilika mioyoni mwenu na pia maishani mwenu. Lakini yupo mwingine ajaye baada yangu, mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, huyo atafanya mengi zaidi yangu. Nami niliye mtumwa wa chini kabisa sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. Yeye huyo atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
“Mimi nawabatiza kwa maji kama ishara kwamba mmetubu dhambi zenu. Lakini baada yangu anakuja aliye mkuu kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuchukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.