Akamwambia Yesu, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe mpaka chini! Kwani Maandiko yanasema, ‘Mungu atawaamuru malaika zake wakusaidie, na mikono yao itakupokea, ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.’”
akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa kuwa imeandikwa, ‘Atawaagiza malaika wake wakuhudumie,’ na, ‘Watakuinua juu mikononi mwao ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.’ ”