Lakini ninawaambia, msimkasirikie mtu yeyote kwa sababu mkifanya hivyo mtahukumiwa. Na mkimtukana mtu yeyote, vivyo hivyo mtahukumiwa na baraza kuu. Na ukimwita mtu kuwa ni mjinga, utakuwa katika hatari ya kutupwa kwenye moto wa Jehanamu.
Lakini mimi nawaambia kwamba, ye yote atakayemkasirikia ndugu yake atasta hili hukumu; na ye yote atakayemtukana ndugu yake, atashtakiwa katika baraza; na ye yote atakayemwambia ndugu yake, ‘Wewe mjinga,’ atastahili hukumu ya moto wa Jehena.