Mwanga wa taa hautang'aa ndani yako tena. Sauti za maarusi hazitasikika ndani yako tena. Wafanyabiashara wako walikuwa watu wakuu wa ulimwengu. Mataifa yote yalidanganyika kwa uchawi wako.
Na nuru ya taa haitaangaza ndani yako tena; Wala sauti ya bwana harusi na bibi harusi haitasikiwa ndani yako kamwe. Maana wafanya biashara wako walikuwa watu maarufu wa duniani, na mataifa yote yalidanganyika kwa uchawi wako.