Kisha nikaanguka chini mbele miguuni pa malaika ili nimwabudu. Lakini malaika akaniambia, “Usiniabudu! Mimi ni mtumishi kama wewe na ndugu zako na dada zako walio na ushuhuda kuhusu Yesu Kristo. Hivyo mwabudu Mungu! Kwa sababu ushuhuda kuhusu Yesu ndiyo roho ya unabii.”
Ndipo nikaanguka kifudifudi miguuni pake kumwabudu, lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi pamoja na wewe na ndugu zako wanaoshikilia ushuhuda wao kwa Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ushuhuda wa Yesu ndio kiini cha unabii.”