Nikajibu, “Wewe unajua ni akina nani, bwana.” Mzee akasema, “Hawa ni wale waliokuja kutokana na mateso makuu. Wamefua kanzu zao kwa kutumia damu ya Mwanakondoo, wako safi na ni weupe.
Nikamjibu, “Bwana, wewe ndiye unayefahamu.” Naye akasema, “Hawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu; wameosha mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo yakawa meupe kabisa.