Malaika wa nne alipopuliza tarumbeta yake. Theluthi ya jua, theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota vikapigwa. Hivyo theluthi moja yao vikawa giza. Theluthi moja ya mchana na usiku ikakosa mwanga.
Kisha malaika wa nne akapiga tarumbeta, na theluthi moja ya jua, theluthi moja ya mwezi na theluthi moja ya nyota, zika pigwa. Kwa hiyo theluthi moja ya mwanga wao ukawa giza. Theluthi moja ya mchana ilikuwa haina mwanga na pia theluthi moja ya usiku.