Watu wengine duniani hawakufa kwa mapigo haya. Lakini watu hawa bado hawakubadili mioyo yao na kuacha kuabudu vitu walivyovitengeneza kwa mikono yao wenyewe. Hawakuacha kuabudu mapepo na sanamu zilizotengenezwa kwa dhahabu, fedha, shaba, mawe na miti, vitu ambavyo haviwezi kuona, au kusikia au kutembea.
Wanadamu waliosalia, ambao hawakuuawa katika maafa hayo, bado walikataa kutubu na kuacha kuabudu vitu walivyotengeneza kwa mikono yao wenyewe. Waliendelea kuabudu pepo, sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, sanamu zisizoweza kuona, kusikia wala kutembea.