Tunajua ya kwamba, kile ambacho sheria inasema ni kwa ajili ya wale waliopewa sheria. Hii inamaanisha kuwa watu wote, Wayahudi na wasio Wayahudi, hawana udhuru kwa matendo yao. Hivyo ulimwengu wote unasimama mbele za Mungu na lazima ujibu kwake.
Basi tunafahamu ya kwamba maagizo yote ya sheria ya Musa yanawahusu wale walio chini ya sheria hiyo. Kusudi la sheria ni kuwafanya watu wote wasiwe na kisingizio na kuuweka ulimwengu wote chini ya hukumu ya Mungu.