Font Size
Warumi 3:25-26
Mungu alimtoa Yesu kama njia ya kusamehe dhambi za watu kupitia imani katika yeye. Mungu anasamehe watu kwa sababu sadaka ya damu ya Yesu iliwaweka huru na dhambi zao. Mungu alimtoa Yesu kuonesha kuwa hutenda haki na bila upendeleo. Alikuwa sahihi huko nyuma alipovumilia na hakuwaadhibu watu kwa sababu ya dhambi zao. Na katika wakati wetu bado anatenda haki. Mungu alifanya hili ili awahukumu watu pasipo kuwa na upendeleo na kumwesabia haki mtu yeyote aliye na imani katika Yesu.
Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwani kwa uvumilivu wake hakuziadhibu dhambi za zamani.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU) © 2017 Bible League International; Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU) © 2017 Bible League International; Neno: Bibilia Takatifu (SNT) Copyright © 1989 by Biblica