Rafiki wapendwa, nilitaka sana kuwaandikia kuhusu wokovu tunaoshiriki pamoja. Lakini nimejisikia kuwa ni muhimu niwaandikie kuhusu kitu kingine: Ninataka kuwatia moyo kuipigania kwa nguvu imani ambayo Mungu aliwapa watakatifu wake. Mungu alitoa imani hii mara moja na ni nzuri wakati wote.
Wapendwa, ingawa nilikuwa na hamu kubwa kuwaandikieni kuhusu wokovu wetu, nimeona ni muhimu niwaandikieni nikiwasihi mwendelee kuipigania kwa nguvu imani ambayo Mungu amewakabidhi watakatifu mara moja tu kwa wakati wote.