Baadhi ya watu wamejiingiza kwa siri kwenye kundi lenu. Watu hawa wamekwisha kuhukumiwa kuwa wakosaji kwa sababu ya matendo yao. Zamani zilizopita manabii waliandika kuhusu watu hao. Wako kinyume na Mungu. Wameigeuza neema ya Mungu kujihalalishia kutenda chochote wanachotaka. Wanakataa kumtii Mkuu aliye peke yake, Bwana wetu Yesu Kristo.
Hii ni kwa sababu watu wasiomcha Mungu ambao tangu zamani wamekwisha kuandikiwa hukumu hii, wamejiingiza miongoni mwenu kwa siri. Hawa ni watu ambao wanapotosha neema ya Mungu wetu na kuitumia kama kisingizio cha kutenda maovu. Wao wanamkana Yesu Kristo ambaye pekee ndiye Mkuu na Bwana wetu.