Walio wema wana vitu vizuri vilivyotunzwa katika mioyo yao. Ndiyo maana husema mambo mazuri. Lakini wale walio waovu wana mioyo iliyojaa uovu, na ndiyo sababu husema mambo maovu.
Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutokana na hazina ya wema uliohifadhiwa ndani yake; na mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutokana na hazina ya uovu uliohifadhiwa ndani yake.