Font Size
Ufunuo 8:13
Nilipokuwa ninatazama, nilimsikia tai aliyekuwa anaruka juu sana angani akisema kwa sauti kuu, “Ole! Ole! Ole kwa wale wanaoishi duniani! Shida kuu zitaanza baada ya sauti za tarumbeta ambazo malaika wengine watatu watapuliza.”
Halafu tena nikatazama, nikasikia tai mmoja akipiga kelele kwa sauti kuu wakati akiruka katikati ya mbingu, “Ole wao! Ole wao! Ole wao watu waishio duniani wakati itakaposikika milio ya tarumbeta ambazo karibuni zitapigwa na malaika watatu waliobakia.”
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU) © 2017 Bible League International; Neno: Bibilia Takatifu (SNT) Copyright © 1989 by Biblica