Previous Prev Day Next DayNext

Bible in 90 Days

An intensive Bible reading plan that walks through the entire Bible in 90 days.
Duration: 88 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Luka 10:1-20:19

10 Baada ya hayo, Yesu akawachagua wafuasi wengine sabini na wawili akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda. Akawaambia, “Mavuno ni mengi lakini wafanya kazi ni wachache, kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno awapeleke wavunaji zaidi katika shamba lake. Haya, nendeni. Ninawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu. Msichukue mkoba wala mfuko, wala viatu; na msipoteze muda kumsalimu mtu ye yote njiani. Mkiingia nyumba yo yote kwanza semeni, ‘Amani iwe kwenu.’ Kama aishiye humo ni mwenye kupenda amani basi baraka hiyo itakaa naye, la sivyo, itawarudia. Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa kile watakachowapa kwa sababu kila mfany akazi anastahili kulipwa mshahara. Msihamehame kutoka nyumba hadi nyumba. Mkienda katika mji mkapokelewa: kuleni mtakachoandal iwa; waponyeni wagonjwa na waambieni: ‘Ufalme wa Mungu umekuja karibu yenu.’

10 “Lakini mkiingia katika mji msikaribishwe, nendeni katika mitaa yake mkaseme: 11 ‘Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoko miguuni mwetu tunayakung’uta juu yenu; lakini fahamuni ya kwamba Ufalme wa Mungu umekuja karibu yenu!’ 12 “Nawahakikishia kwamba siku ile Mungu atakapouhukumu ulimwengu adhabu ya Sodoma itakuwa nafuu kuliko ya mji huo! 13 Ole wenu watu wa Korazini na wa Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifany ika Tiro na Sidoni watu wa huko wangalitubu zamani, wakivaa magu nia na kujimwagia majivu kama dalili ya majuto. 14 Lakini siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Tiro na Sidoni kuliko kwenu. 15 Na ninyi je, watu wa Kapernaumu, mnafikiri mtainuliwa juu hadi mbinguni? La, Mungu atawatupa chini hadi kuzimuni. 16 “Ye yote atakayewasikiliza ninyi amenisikiliza mimi, naye awakataaye amenikataa. Lakini anikataaye mimi amemkataa yeye aliyenituma.”

17 Wale wanafunzi sabini na wawili wakarudi wakiwa na furaha. Wakamwambia Yesu, “Bwana, tukilitumia jina lako, hata pepo wanatutii!” 18 Akawajibu, “Nimemwona shetani akianguka kama radi kutoka mbinguni. 19 Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na kushinda nguvu zote za yule adui; wala hakuna kitu cho chote kitakachoweza kuwadhuru. 20 Lakini msifurahi kwa kuwa pepo wanawatii, ila furahini kwa kuwa majina yenu yamean dikwa mbinguni.”

21 Wakati huo, Yesu akiwa amejawa na furaha ya Roho Mtaka tifu, akasema, “Ninakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa sababu mambo haya ambayo umewaficha wenye elimu na wenye hekima umependa kuwafunulia wale wakuaminio kama watoto wadogo. Na haya yote yamefanyika kwa mapenzi yako Baba. 22 Baba yangu amenika bidhi mambo yote. Hakuna anayemfahamu Mwana isipokuwa Baba: na hakuna anayemfahamu Baba isipokuwa Mwana na wale ambao Mwana ame penda humdhihirisha Baba kwao.” 23 Basi Yesu akawageukia wana funzi wake akawaambia faraghani, “Mmebarikiwa kuona mambo haya mnayoyaona! 24 Nawaambie ni kweli, manabii wengi na wafalme wal itamani kuona mnayoyaona na kusikia mnayoyasikia lakini hawaku pata nafasi hiyo.” Mfano Wa Msamaria Mwema

25 Mwalimu mmoja wa sheria alisimama akajaribu kumpima Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?” 26 Yesu akamjibu, “Sheria inasemaje? Unaitafsiri vipi?” 27 Yule mwalimu wa sheria akajibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote. Na umpende jirani yako kama unavyojipenda mwe nyewe.” 28 Yesu akamwambia, “Jibu lako ni sahihi. Fanya hivyo nawe utaishi.” 29 Lakini yule mwalimu wa sheria akitaka kuon yesha kwamba hoja yake ilikuwa na maana zaidi, akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”

30 Yesu akamjibu, “Mtu mmoja aliteremka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Njiani akashambuliwa na majambazi; wakamwibia kila kitu alichokuwa nacho, wakampiga wakamwacha karibu ya kufa. 31 litokea kwamba kuhani mmoja alikuwa anapitia njia ile. Ali pomwona huyo mtu, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo. 32 Vivyo hivyo Mlawi mmoja naye alipopita, alimwona, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo.

33 “Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri kupitia njia hiyo alipomkuta, alimwonea huruma, 34 akamwendea akasafisha maj eraha yake kwa divai na mafuta, akayafunga. Kisha akamweka kwenye punda wake akaenda naye mpaka nyumba ya wageni ambapo alimtunza. 35 Kesho yake, yule Msamaria alipokuwa anaondoka, akampa mwenye nyumba ya wageni fedha akamwomba amtunze yule mgonjwa na akaahidi kulipa gharama yo yote ya ziada atakaporudi.

36 “Unadhani ni yupi kati ya hawa watatu alikuwa jirani yake yule mtu aliyeshambuliwa na majambazi?”

37 Yule mwalimu wa sheria akajibu, “Ni yule aliyemwonea huruma.” Yesu akasema, “Nenda ukafanye vivyo hivyo.”

Yesu Awatembelea Martha na Mariamu

38 Wakati Yesu na Wanafunzi wake walipokuwa wakiendelea na safari yao ya kwenda Yerusalemu, walifika katika kijiji kimoja ambapo mwanamke mmoja aliyeitwa Martha alimkaribisha Yesu nyum bani kwake. 39 Martha alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Mariamu ambaye aliketi chini karibu na Yesu akisikiliza mafundisho yake.

40 Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote. Kwa hiyo alikuja kwa Yesu akalalamika, “Bwana, hujali kwamba mdogo wangu ameniachia kazi zote? Mwambie aje anisaidie!” 41 Bwana akamjibu, “Martha! Martha! Mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? 42 Unahitaji kujua kitu kimoja tu. Mariamu amechagua kil icho bora, na hakuna mtu atakayemnyang’anya.” Yesu Awafundisha Wanafunzi Wake Kuomba

11 Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomal iza, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tafadhali tufundishe kuomba kama Yohana Mbatizaji alivyowafundisha wana funzi wake.” Akawaambia, “Mnapoomba, semeni hivi: Baba, Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje. Utupatie chakula chetu kila siku. Utusamehe dhambi zetu kwa kuwa na sisi tunawasamehe wote wanaotukosea. Na usitutie katika majaribu.” Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu ana rafiki yake. Akamwendea usiku wa manane akamwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu. Nimefikiwa na rafiki yangu akiwa safarini nami sina chakula cha kumpa.’ Yule aliyeko ndani akajibu, ‘Usinisumbue! Nimekwisha kufunga mlango. Na mimi na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka kukupa cho chote.’ “Nawaambieni, hata kama huyo mtu hataamka na kumpa mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ameendelea kuomba bila kukata tamaa ataamka ampe kiasi anachohitaji. Kwa hiyo nawaambia, ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa mlango. 10 Kwa kuwa kila anayeomba hupewa; naye atafutaye, hupata; na kila abishaye, hufunguliwa mlango. 11 “Ni baba yupi miongoni mwenu, ambaye mtoto wake akimwomba samaki, atampa nyoka badala yake? 12 Au akimwomba yai atampa nge? 13 Ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho

Yesu Na Beelzebuli

14 Yesu alikuwa anamtoa pepo mtu mmoja ambaye alikuwa bubu. Pepo huyo alipotoka, yule mtu akaanza kusema! Watu wakashangaa. 15 Lakini wengine wakasema: “Anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzeb uli, yule mkuu wa pepo wote.” 16 Wengine wakamjaribu kwa kum womba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

17 Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, “Nchi yo yote iliyo na mgawanyiko wa vikundi-vikundi vinavyopingana au familia yenye mafarakano, huangamia. 18 Kama ufalme wa shetani ungekuwa umega wanyika wenyewe kwa wenyewe ungesimamaje? Nasema hivi kwa sababu mnasema ninaondoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli. 19 Kama mimi ninaondoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu je, wao huwaondoa pepo kwa uwezo wa nani? Wao watawaamulia. 20 Lakini kwa kuwa ninaondoa pepo kwa uwezo wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umewajia. 21 Mtu mwenye nguvu aliye na silaha anapoilinda nyumba yake, mali yake ni salama. 22 Lakini mtu mwenye nguvu zaidi akimshambulia na kumshinda, atamnyang’anya silaha alizozitegemea na kugawanya mali yote. 23 “Mtu ambaye hayuko upande wangu, anapingana nami, na mtu asiyekusanya pamoja nami, anatawanya.

24 “Pepo mchafu akimtoka mtu, anazunguka jangwani akitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata anasema, ‘Kwa nini nisirudi kwe nye nyumba yangu niliyotoka?’ 25 Akirudi, na kuikuta ile nyumba ni safi na imepangwa vizuri, 26 huenda kuwaleta pepo wengine saba wachafu kuliko yeye wakaingia na kuishi humo. Na hali ya sasa ya mtu huyo inakuwa mbaya kuliko ya kwanza.”

27 Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika umati akasema kwa nguvu, “ Amebarikiwa mama aliyekuzaa na kukunyon yesha.” 28 Yesu akajibu, “Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulifuata.”

Ishara Ya Yona

29 Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu aliendelea kufundisha akisema, “Watu wa kizazi hiki ni waovu. Wanatafuta ishara lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. 30 Kwa maana kama Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo mimi Mwana wa Adamu nitakavyokuwa ishara kwa kizazi cha sasa. 31 Siku ya hukumu malkia wa Sheba atashuhudia kwamba watu wa sasa wana hatia kwa sababu yeye alisafiri kutoka mbali kuja kusikiliza hekima ya Sulemani. Lakini sasa, aliye mkuu kuliko Sulemani yuko hapa. 32 Siku ile ya hukumu, watu wa Ninawi watashuhudia kwamba watu wa sasa wana hatia kwa sababu Yona ali powahubiria waliacha dhambi zao. Lakini sasa aliye mkuu kuliko

Taa Ya Mwili

33 “Hakuna mtu awashaye taa akaificha au kuifunika, ila huiweka mahali pa juu ili watu wote wanaoingia waone nuru yake. 34 Jicho lako ni nuru ya mwili wako. Macho yakiwa mazima huan gaza mwili wako wote; lakini yakiwa mabovu, mwili wako pia uta kuwa katika giza. 35 Kwa hiyo hakikisha kwamba una nuru ndani yako, wala si giza. 36 Ikiwa mwili wako wote una nuru, bila sehemu yo yote kuwa gizani, basi utang’aa kabisa kama inavyokuwa wakati taa inapokuangazia.”

Yesu Awaonya Mafarisayo Na Wanasheria

37 Yesu alipomaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimkaribisha nyumbani kwake kwa chakula. Yesu akaingia na kuketi chakulani moja kwa moja. 38 Farisayo yule alipoona kwamba Yesu hakunawa kwanza kabla ya kula alishangaa. 39 Ndipo Bwana akamwambia, “Ninyi Mafarisayo mnasafisha kikombe na sahani kwa nje huku ndani mmejaa udhalimu na uovu. 40 Wajinga Ninyi! Hamjui kuwa yeye aliyetengeneza sehemu ya nje ndiye aliyetengeneza na ya ndani pia? 41 Watendeeni ukarimu maskini kwa kuwapa vilivyomo ndani ya vikombe na sahani zenu na kila kitu kitakuwa safi kwenu.

42 “Lakini ole wenu, Mafarisayo! Ninyi mnamtolea Mungu sehemu ya kumi ya mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga lakini mnapuuza haki na kumpenda Mungu. Mngeweza kutoa matoleo hayo pasipo kusahau haki na upendo kwa Mungu.

43 “Ole wenu, Mafarisayo! Ninyi mnapenda kuketi viti vya mbele katika masinagogi na kusalimiwa kwa heshima masokoni! 44 Ole wenu! Kwa maana ninyi ni kama makaburi yasiyokuwa na alama, ambayo watu huyakanyaga pasipo kujua.”

45 Mwalimu mmoja wa sheria akasema, “Mwalimu, unapozungumza hivyo unatushutumu na sisi wanasheria!” 46 Yesu akamjibu, “Hata ninyi wanasheria, ole wenu! Mnawabebesha watu mzigo wa sheria ambazo hawawezi kuzitimiza; wala hamfanyi lo lote kuwa saidia iwe rahisi kwao kuzitimiza. 47 Ole wenu kwa kuwa mnawa jengea makaburi manabii waliouawa na babu zenu. 48 Kwa kufanya hivyo mnakiri kwamba mnaunga mkono kitendo hicho walichofanya babu zenu. Wao waliua na ninyi mnatengeneza makaburi.

49 “Ndio maana Mungu katika hekima yake alisema, ‘Nita wapeleka manabii na mitume, na baadhi yao watawaua na wengine watawatesa.’ 50 Kwa hiyo damu ya manabii wote iliyomwagika tangu mwanzo wa dunia itahesabiwa juu ya watu wa kizazi hiki; 51 tangu damu ya Abeli mpaka damu ya Zakaria aliyeuawa kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Nawaambia kweli, watu wa kizazi hiki wataadhibiwa kwa ajili yao wote. 52 Ole wenu ninyi wanashe ria kwa maana mmeuchukua ufunguo unaofungua nyumba ya maarifa. Ninyi wenyewe hamkuingia na wale waliokuwa wanaingia mkawazuia.”

53 Yesu alipoondoka hapo, walimu wa sheria na Mafarisayo wakawa wanampinga vikali na kumwuliza maswali mengi, 54 wakijar ibu kumtega ili aseme kitu ambacho watakitumia kumshitaki.

Yesu Awaonya Na Kuwafariji Wanafunzi

12 Wakati huo, maelfu ya watu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu alizungumza na wanafunzi wake kwanza, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani, unafiki wao.

“Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.

“Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi. Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: mwogopeni yule ambaye baada ya kumwua mtu ana mamlaka ya kumtupa motoni. Naam: huyo, mwogopeni! Mnajua kwamba mbayuwayu watano huuzwa kwa bei ndogo sana. Lakini Mungu anamjali kila mmoja wao. Mungu anafahamu hata idadi ya nywele zilizoko katika vichwa vyenu. Kwa hiyo msiogope: ninyi mna thamani zaidi kuliko mbayuwayu wengi. “Ninawaambia, kila atakayenikiri mbele za watu, pia mimi Mwana wa Adamu nitamkiri mbele ya malaika wa Mungu. Lakini kila anayenikana mbele za watu, pia mimi Mwana wa Adamu nitamkana mbele ya malaika wa Mungu. 10 Na kila atakayesema neno baya kunihusu mimi Mwana wa Adamu atasamehewa. Lakini mtu anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. 11 “Na watakapowapeleka katika masinagogi mbele ya watawala na mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu mtakavyojitetea au mtakavyosema: 12 kwa maana wakati huo Roho Mtakatifu atawafundisha mnachopaswa kusema.”

Mtakatifu atawafundisha mnachopaswa kusema.”

13 Na mtu mmoja katika umati akasema, “Bwana, mwambie ndugu yangu anigawie urithi aliotuachia baba yetu.” 14 Yesu akamwam bia, Rafiki, ni nani aliyenifanya mimi niwe hakimu wenu au mga wanyaji wa urithi wenu?” 15 Ndipo akawaambia, “Jihadharini na jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana uhai wa mtu hautokani na wingi wa mali aliyo nayo.”

16 Kisha akawaambia mfano, “Shamba la tajiri mmoja lilizaa sana. 17 Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Maana sina mahali pa kuweka mavuno yangu.’ 18 Kisha akasema, ‘Nitafanya hivi: nitabomoa maghala yangu na kujenga maghala makubwa zaidi na huko nitaweka mavuno yangu yote na vitu vyangu. 19 Na nitasema moy oni, ‘Hakika nina bahati! Ninayo mali ya kunitosha kwa miaka mingi. Sasa nitapumzika: nile, ninywe na kustarehe.’ 20 Lakini Mungu akamwambia, ‘Mjinga wewe! Usiku huu huu utakufa! Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea vitakuwa vya nani?’ 21 Hivi ndivyo itakavy okuwa kwa mtu ye yote anayehangaika kujikusanyia utajiri duniani lakini si tajiri mbinguni kwa Mungu.”

22 Kisha akawaambia wanafunzi wake, “Kwa hiyo ninawaambia, msihangaikie maisha yenu, kwamba mtakula nini; au miili yenu kwamba mtavaa nini. 23 Uhai ni zaidi ya chakula; na mwili ni zaidi ya mavazi. 24 Chukueni mfano wa kunguru! Wao hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala po pote pa kuweka nafaka, lakini Mungu anawalisha. Ninyi ni bora zaidi kuliko ndege! 25 Na ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha anaweza kujiongezea urefu wa maisha yake hata kwa saa moja? 26 Kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo; kwa nini basi mhangaikie hayo mengine? 27 Yata zameni maua yanavyostawi: hayafanyi kazi, wala kujitengenezea nguo; lakini ninawaambia, hata Sulemani katika ufahari wake wote, hakuwahi kuvishwa vizuri kama ua mojawapo! 28 Ikiwa Mungu huyav isha hivi majani ambayo leo yapo shambani na kesho yanachomwa moto; ataachaje kuwavisha ninyi hata zaidi? Mbona mna imani ndogo! 29 Wala msihangaike mtakula nini au mtakunywa nini. Msiwe na wasiwasi juu ya haya. 30 Watu wasiomjua Mungu huhan gaika sana juu ya vitu hivi. Lakini Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnavihitaji. 31 Basi, tafuteni Ufalme wa Mungu; na hivyo vyote atawapatia.”

32 “Ninyi kundi dogo, msiogope kwa maana Mungu amependa mtawale naye katika ufalme wake. 33 Uzeni mali zenu muwape mas kini; ili mjipatie mikoba isiyochakaa, na kujiwekea hazina mbin guni ambapo mwizi hafiki wala nondo haharibu. 34 Kwa maana unapoiweka akiba yako ndipo na moyo wako utakapokuwa.”

Kukesha

35 “Muwe tayari mkiwa mmevaa, na taa zenu zikiwaka. 36 Muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka haru sini, ili atakapokuja na kugonga mlango wamfungulie mara moja. 37 Itakuwa ni heri kwa wale watumishi ambao bwana wao akija ata wakuta wanamngoja. Nawaambieni kweli, atajiandaa na kuwaketisha karamuni awahudumie. 38 Itakuwa ni furaha kubwa kwao ikiwa ata wakuta tayari hata kama atakuja usiku wa manane au alfajiri.

39 Fahamuni kwamba kama mwenye nyumba angalijua ni saa ngapi mwizi atakuja, angalijiandaa asiiachie nyumba yake ivunjwe. 40 Kwa hiyo, ninyi pia mkae tayari, kwa maana mimi Mwana wa Adamu nita kuja saa ambayo hamnitegemei.”

Mtumishi Mwaminifu Na Asiye mwaminifu

41 Ndipo Petro akamwambia, “Bwana, mfano huu unatuambia sisi peke yetu au watu wote?” 42 Yesu akamwambia, “Ni yupi wakili mwaminifu na mwenye busara? Ni yule ambaye bwana wake atamfanya mtawala juu ya nyumba yake yote naye awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa. 43 Itakuwa ni furaha kwa mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 44 Ninawahakikishia kwamba atampa mamlaka juu ya vyote alivyo navyo. 45 Lakini kwa mfano, kama yule mtumishi atawaza moyoni mwake, ‘Bwana wangu anachelewa kurudi,’ halafu aanze kuwa piga wale watumishi wa kiume na wa kike, na kula na kunywa na kulewa, 46 bwana wake atarudi siku ambayo hakumtazamia, na saa asiyoijua. Huyo bwana wake atamwadhibu vikali pamoja na wote wasiotii. 47 Na mtumishi ambaye anafahamu mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, pia ataad hibiwa vikali. 48 Lakini mtumishi ambaye hafahamu anachotakiwa kufanya na akafanya kitu kinachostahili adhabu, atapata adhabu ndogo. Mungu atatarajia vingi kutoka kwa mtu aliyepewa vipawa vingi; na mtu aliyekabidhiwa vingi zaidi, atadaiwa zaidi pia.”

49 “Nimekuja kuleta moto duniani! Laiti kama dunia inge kuwa tayari imeshawaka! 50 Lakini kuna ubatizo ambao lazima niu pokee na dhiki yangu ni kuu mpaka ubatizo huo utakapokamilika.

51 “Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambieni sivyo; nimekuja kuleta mafarakano. 52 Kuanzia sasa, katika nyumba ya watu watano kutakuwa na mgawanyiko: watatu wakipingana na wawili, na wawili wakipingana na watatu. 53 Baba atapingana na mwanae na mwana atapingana na babaye; mama atapingana na bin tiye na binti atapingana na mamaye; mama mkwe atapingana na mke wa mwanae ambaye naye atapingana na mama mkwe wake.”

Kutambua majira

54 Kisha Yesu akawaambia watu, “Mkiona wingu likitokea mag haribi, mara moja mnasema, ‘Mvua hiyo inakuja!’ na inakuwa hivyo. 55 Na mnapouona upepo wa kusi ukivuma, mnasema, ‘Kutakuwa na joto!’ Na linakuwepo. 56 Enyi wanafiki! Mnaweza kutambua dalili za hali ya hewa; kwa nini basi hamtambui maana ya mambo yanayoto kea sasa? 57 Kwa nini hamuamui lililo haki kutenda? 58 Kama mtu akikushtaki mahakamani, jitahidi sana kupatana na mshtaki wako wakati mkiwa mnaenda mahakamani, ili asikufikishe mbele ya hakimu, na hakimu akakukabidhi kwa polisi, na polisi wakakutia gerezani. 59 Nakuhakikishia kwamba, hutatoka huko gerezani mpaka umelipa faini yote.”

13 Wakati huo, watu fulani walimwambia Yesu habari za Wagali laya ambao Pilato aliwaua na damu yao akaichanganya na damu ya sadaka waliyokuwa wakimtolea Mungu. Yesu akawajibu, “Mnadhani Wagalilaya hao walikufa kifo cha namna hiyo kwa kuwa walikuwa na dhambi kuwazidi Wagalilaya wengine wote? Sivyo hata kidogo. Ninyi pia msipoacha dhambi zenu mtaangamia vivyo hivyo. Au wale watu kumi na wanane ambao walikufa walipoangukiwa na mnara huko Siloamu, mnadhani wao walikuwa waovu kuliko watu wote waliokuwa wanaishi Yerusalemu? Nawaambieni, sivyo! Ninyi pia msipoacha dhambi zenu, mtaangamia vivyo hivyo.”

Mfano Wa Mti Usiozaa Matunda

Kisha Yesu akatoa mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini uliopandwa katika shamba lake la mizabibu, akaenda kutafuta tini kwenye mti huo asipate hata moja. Kisha akamwambia mtunza shamba:, ‘Kwa muda wa miaka mitatu sasa nimekuwa nikija kutafuta matunda kwenye mtini huu, sijawahi kupata hata moja. Ukate, sioni kwa nini uendelee kutumia ardhi bure!’ Yule mtunza shamba akam jibu, ‘Bwana, tuuache tena kwa mwaka mmoja zaidi, niulimie, niuwekee mbolea. Ukizaa matunda, vema; na usipozaa baada ya hapo, utaukata.”’ Yesu Amponya Mwanamke Siku Ya Sabato

10 Siku moja ya sabato, Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. 11 Na hapo alikuwapo mwanamke mmoja alikuwa ameugua kwa muda wa miaka kumi na minane kutokana na pepo ali yekuwa amemwingia. Hali hiyo ilimfanya mwanamke huyo apindike hata asiweze kusimama wima. 12 Yesu alipomwona, akamwita akam wambia, “Mama, uwe huru, umepona ugonjwa wako.” 13 Yesu akamwekea mikono, na mara akasimama wima, akamtukuza Mungu. 14 Mkuu wa sinagogi akakasirika kwa kuwa Yesu alikuwa ameponya mtu siku ya sabato. Kwa hiyo akawaambia watu, “Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi, katika siku hizo, njooni mpo nywe; msije kuponywa siku ya sabato!”

15 Lakini Bwana akamjibu, “Ninyi ni wanafiki! Kila mmoja wenu humfungulia ng’ombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya sabato. 16 Je, huyu mama, ambaye ni binti wa Ibrahimu aliyefungwa na shetani kwa miaka yote hii kumi na minane, hastahili kufunguliwa kutoka katika kifungo hicho siku ya sabato?” 17 Aliposema haya, wapinzani wake wakaona aibu lakini watu wakafurahi kwa ajili ya mambo ya ajabu aliyoyafanya. Mfano Wa Punje Ya Haradali

18 Kisha Yesu akauliza, “Ufalme wa Mungu ukoje? Nitaufanan isha na nini? 19 Umefanana na punje ndogo sana ya haradali ambayo mtu aliichukua akaipanda katika shamba lake, ikamea, ikawa mti na ndege wa angani wakatengeneza viota vyao kwenye matawi yake.”

Mfano Wa Hamira

20 Yesu akauliza tena, “Nitaufananisha na nini Ufalme wa Mungu? 21 Uko kama hamira ambayo mwanamke aliichukua na kuichan ganya kwenye vipimo vitatu vya unga wa ngano na wote ukaumuka.”

Mlango Mwembamba

22 Yesu akapita katika miji na vijiji akifundisha wakati akisafiri kwenda Yerusalemu. 23 Mtu mmoja akamwuliza, “Bwana, ni watu wachache tu watakaookolewa?” 24 Akajibu, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana, nawaambia, wengi watataka kuingia na hawataweza. 25 Wakati mwenye nyumba ataka poamka na kufunga mlango, mtasimama nje mkigonga mlango na kusema, ‘Bwana utufungulie!’ Atawajibu, ‘Sijui mtokako!’ 26 Nanyi mtamjibu, ‘Tulikula na kunywa pamoja nawe, ulifundisha katika mitaa yetu!’ 27 Lakini yeye atawajibu, ‘Sijui mtokako. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’ 28 Ndipo kutakuwapo na kilio na kusaga meno mtakapomwona Ibrahimu, Isaka na Yakobo na manabii wote wakiwa katika Ufalme wa Mungu, wakati ninyi mkiwa mmetupwa nje. 29 Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi na kaskazini na kusini na wataketi kwenye sehemu walizoandaliwa kar amuni katika Ufalme wa Mungu. 30 Hakika wapo watu ambao sasa wako mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wengine walio wa kwanza sasa watakaokuwa wa mwisho.” Yesu Aomboleza Juu Ya Yerusalemu

31 Wakati huo huo baadhi ya Mafarisayo wakamwendea Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine kwa maana Herode anataka kukuua.” 32 Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie yule mbweha: ninafukuza pepo na kuponya wagonjwa leo na kesho, na siku ya tatu nitakamilisha kazi yangu. 33 Sina budi kuendelea na safari yangu leo, kesho na kesho kutwa, kwa maana haiwezekani nabii kufa mahali pengine isipokuwa Yerusalemu.

34 “Ewe Yerusalemu, Yerusalemu, wewe uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwa kusanya watoto wako pamoja kama kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hukuniruhusu! 35 Sasa nyumba yako inaachwa tupu. Ninakuambia, hutaniona tena mpaka wakati ule uta kaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye katika jina la Bwana.”’

14 Siku moja ya sabato Yesu alipokuwa amekwenda kula chakula kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo, watu walikuwa wakimtazama kwa makini. Mtu mmoja mwenye ugonjwa wa kuvimba miguu na mikono akaja mbele yake. Yesu akawauliza walimu wa sheria na Mafari sayo, “Je, sheria inaruhusu kumponya mtu siku ya sabato au hairuhusu?” Wakakaa kimya. Basi Yesu akamshika yule mgonjwa akamponya, akamruhusu aende zake. Kisha akawauliza, “Kama mmoja wenu angekuwa na mtoto au ng’ombe wake ambaye ametumbukia katika kisima siku ya sabato, hamtamvuta mara moja na kumtoa?” Hawakuwa na la kujibu.

Alipoona jinsi wageni walioalikwa walivyokuwa wakichagua viti vya wageni wa heshima, akawaambia mfano huu: “Mtu akiku alika harusini, usikae kwenye kiti cha mgeni wa heshima. Inaweze kana kuwa amealika mheshimiwa akuzidiye, na yule aliyewaalika ninyi wawili akaja kukuambia, ‘Tafadhali mpishe huyu bwana.’ Ndipo kwa aibu utalazimika kwenda kukaa katika kiti cha nyuma kabisa. 10 Badala yake, unapoalikwa, chagua kiti cha nyuma; na mwenyeji wako akikuona atakuja akuambie, ‘Rafiki yangu, njoo kwe nye nafasi ya mbele zaidi.’ Kwa jinsi hii utakuwa umepewa heshima mbele ya wageni wote. 11 Kwa maana kila mtu anayejitukuza atash ushwa naye ajishushaye atatukuzwa.”

12 Kisha Yesu akamwambia yule aliyewaalika, “Uandaapo kar amu ya chakula cha mchana au jioni, usialike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako tajiri; ukifanya hivyo wao nao watakualika kwao na hivyo utakuwa umelipwa kwa kuwaalika. 13 Bali ufanyapo karamu, waalike maskini, vilema na vipofu; 14 nawe utapata baraka kwa sababu hawa hawana uwezo wa kukulipa.

Mfano Wa Karamu Ya Ufalme Wa Mbinguni

15 Mmoja wa wale waliokuwa mezani pamoja naye aliposikia maneno haya akamwambia, “Ana heri mtu atakayepata nafasi ya kula katika karamu ya Ufalme wa Mbinguni!” 16 Yesu akamjibu, ‘ ‘Mtu mmoja alikuwa anaandaa karamu kubwa, akaalika watu wengi. 17 Wakati wa sherehe ulipofika, akamtuma mtumishi wake akawaam bie walioalikwa, ‘Karibuni, kila kitu ni tayari sasa.’ 18 Lakini wote, mmoja mmoja, wakaanza kutoa udhuru. Wa kwanza akasema, ‘ Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’ 19 Mwingine akasema, ‘Nimenunua ng’ombe wa kulimia, jozi tano; nimo njiani kwenda kuwajaribu, tafadhali niwie radhi.’ 20 Na mwingine akasema, ‘Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.’

21 “Yule mtumishi akarudi, akampa bwana wake taarifa. Ndipo yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda upesi kwenye mitaa na vichochoro vya mjini uwalete maskini, vilema, vipofu na viwete.’

22 “Baadaye yule mtumishi akamwambia ‘Bwana, yale uliyon iagiza nimefanya, lakini bado ipo nafasi.’ 23 Ndipo yule bwana akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda kwenye barabara na njia zilizoko nje ya mji uwalazimishe watu waje mpaka nafasi zote zijae. 24 Ninawaambia, hakuna hata mmoja wa wale niliowapelekea mwaliko rasmi atakayeionja karamu yangu.”

Gharama Ya Kuwa Mfuasi Wa Yesu

25 Wakati mmoja umati mkubwa wa watu ulipokuwa ukifuatana na Yesu, yeye aligeuka, akawaambia, 26 “Mtu ye yote anayekuja kwangu hawezi kuwa mfuasi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto, kaka zake na dada zake; naam, hata maisha yake mwenyewe. 27 Na ye yote asiyebeba msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mfuasi wangu.

28 “Ni nani kati yenu ambaye kama anataka kujenga, hatakaa kwanza na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha ujenzi? 29 Kwa maana ikiwa atajenga msingi halafu ashindwe kuendelea, wote watakaouona watamcheka 30 wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga lakini ameshindwa kumal iza!’

31 “Au tuseme mfalme mmoja anataka kwenda vitani kupigana na mfalme mwingine: si atakaa kwanza ajishauri kama yeye na jeshi lake lenye watu elfu kumi ataweza kupigana na yule anayekuja na watu elfu ishirini? 32 Kama hawezi, basi itambidi apeleke wajumbe wakati yule mfalme mwingine bado yuko mbali na kuomba masharti ya amani. 33 Hali kadhalika, hakuna mtu atakayeweza kuwa mfuasi wangu kama hataacha vyote alivyo navyo.”

Chumvi Isiyofaa

34 “Chumvi ni kitu kizuri. Lakini chumvi ikiwa imepoteza ladha yake, haiwezi kuwa chumvi tena. 35 Haifai kuwa udongo wala kuwa mbolea; watu huitupa nje. Mwenye nia ya kusikia na asikie!” Mfano Wa Kondoo Aliyepotea

15 Basi watoza kodi na wenye dhambi wakaja kwa Yesu ili wapate kumsikiliza. Mafarisayo na walimu wa sheria wakaanza kunung’unika, “Huyu mtu anawakaribisha wenye dhambi na kula nao!” Ndipo Yesu akawaambia mfano huu: “Tuseme mmoja wenu ana kondoo mia moja halafu mmoja wao apotee. Si ana waacha wale tisini na tisa malishoni aende kumtafuta huyo aliyepotea mpaka ampate? Akisha kumpata atambeba mabegani mwake na kwenda nyum bani. Kisha atawaita marafiki na majirani na kuwaambia, ‘Fura hini pamoja nami; nimempata kondoo wangu aliyepotea.’ Nawaam bieni, vivyo hivyo kutakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye na kuacha dhambi zake, kuliko ilivyo kwa wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.”

Shilingi Iliyopotea

“Au tuseme mwanamke ana shilingi kumi halafu apoteze moja. Si atawasha taa afagie nyumba na kutafuta kwa uangalifu mpaka aipate? Na akisha kuipata atawaita marafiki zake na majirani na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimeipata ile shilingi yangu iliyopotea!’ 10 Vivyo hivyo nawaambia, kuna furaha mbele ya mal aika wa Mungu kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye na kuacha dhambi.”

Mwana Mpotevu

11 Yesu akaendelea kusema, “Kulikuwa na mtu aliyekuwa na watoto wawili wa kiume. 12 Yule mdogo akamwambia baba yake, ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Basi huyo baba akagawanya mali yake kati yao.

13 “Baada ya muda mfupi yule mdogo akakusanya vitu vyote alivyokuwa navyo akaenda nchi ya mbali akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa. 14 Baada ya kutumia kila kitu alichokuwa nacho, kukawa na njaa kali katika nchi ile yote naye akawa hana cho chote. 15 Kwa hiyo akaomba kibarua kwa raia mmoja wa nchi hiyo aliyemtuma shambani kwake kulisha nguruwe. 16 Akatamani kujish ibisha kwa maganda waliyokuwa wanakula nguruwe, wala hakuna mtu aliyempa cho chote cha kula.

17 “Hatimaye akili zikamrudia, akasema, ‘Ni watumishi wan gapi walioajiriwa na baba yangu ambao wana chakula cha kuwatosha na kusaza nami hapa nakufa kwa njaa! 18 Nitaondoka nirudi kwa baba yangu nikamwambie, ‘Baba, nimetenda dhambi mbele ya Mungu na mbele yako. 19 Sistahili kuitwa mwanao tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.’ 20 Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake. Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanae, akamkumbatia na kumbusu. 21 Yule mtoto akasema, ‘Baba, nimekosa mbele ya Mungu na mbele yako. Sistahili kuitwa mwanao tena.’ 22 Lakini baba yake aka waambia watumishi, ‘Leteni upesi kanzu iliyo bora mumvalishe. Pia mvalisheni pete na viatu. 23 Kisha mleteni yule ndama aliyenona mkamchinje; ili tule tusherehekee. 24 Kwa maana huyu mwanangu alikuwa amekufa, na sasa yu hai tena; alikuwa amepotea na sasa amepatikana.’ Basi wakaanza sherehe.

25 “Wakati huo kaka yake alikuwa shambani. Alipokuwa ana karibia nyumbani akasikia sauti ya nyimbo na ngoma. 26 Akamwita mmoja wa watumishi akamwuliza, ‘Kuna nini?’ 27 Akamwambia, ‘Mdogo wako amekuja, na baba yako amemchinja yule ndama aliyenona kwa sababu amempata mwanawe akiwa mzima.’ 28 Yule kaka akakasi rika, akakataa kuingia ndani. Basi baba yake akaenda nje akaanza kumbembeleza. 29 Lakini yeye akamjibu baba yake, ‘Angalia, miaka yote hii nimekutumikia na hata siku moja sijaacha kutii amri zako, lakini hujanipa hata mwana mbuzi ili nisherehekee na mara fiki zangu. 30 1Lakini huyu mwanao ambaye ametapanya mali yako kwa makahaba amerudi nyumbani nawe umemchinjia ndama aliyenona!’

31 “Baba yake akamwambia, ‘Mwanangu, umekuwa nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako. 32 Lakini ilitubidi tufurahi na kusherehekea kwa sababu mdogo wako alikuwa amekufa na sasa yu hai tena, alikuwa amepotea naye amepatikana.”’ Mfano Wa Meneja Mjanja

16 Akawaambia wanafunzi wake, “Palikuwa na tajiri mmoja na meneja wake. Ilisemekana kwamba huyo meneja alikuwa anatumia vibaya mali ya tajiri yake. Basi huyo tajiri akamwita meneja wake akamwuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayosikia kukuhusu? Nitay arishie hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu kwa maana hutaendelea kuwa meneja tena.’

“Yule meneja akawaza moyoni mwake, ‘Nitafanya nini sasa? Bwana wangu anataka kuniondoa katika kazi yangu. Sina nguvu za kulima, na ninaona aibu kuombaomba! Najua nitakalofanya ili nikipoteza kazi yangu hapa, watu wanikaribishe nyumbani kwao.’

“Kwa hiyo akawaita wadeni wote wa tajiri wake, mmoja mmoja. Akamwuliza wa kwanza, ‘Deni lako kwa bwana wangu ni kiasi gani?’ Akajibu, ‘Galoni mia nane za mafuta ya alizeti.’ Meneja akamwambia, ‘Chukua hati hii ya deni lako, ibadilishe upesi, uan dike mia nne.’ Kisha akamwuliza wa pili, ‘Na wewe deni lako ni kiasi gani?’ Akajibu, ‘Vipimo elfu moja vya ngano.’ Yule meneja akamwambia, ‘ Chukua hati yako, uandike mia nane.’

“Yule tajiri akamsifu yule meneja mjanja kwa jinsi alivy otumia busara. Kwa maana watu wanaojishughulisha na mambo ya dunia hii hutumia busara zaidi kuliko watu wa nuru kukamilisha mambo yao. Nami nawaambieni, tumieni mali ya dunia hii kujipa tia marafiki, ili itakapokwisha mkaribishwe katika makao ya milele.

10 “Mtu ambaye ni mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu hata katika mambo makubwa; na mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa. 11 Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika kutunza mali ya dunia hii, ni nani atakayewaamini awakabidhi mali ya kweli? 12 Na kama ham kuwa waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa mali yenu wenyewe? 13 Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine; au atamheshimu mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na mali.”

14 Basi Mafarisayo, ambao wenyewe walipenda fedha, waliyasi kia hayo yote wakamcheka. 15 Yesu akawaambia, “Ninyi mnajifa nya kuwa wenye haki mbele za wanadamu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana vile vitu ambavyo wanadamu wanavithamini sana, kwa Mungu havina thamani yo yote.”

Sheria Na Ufalme Wa Mungu

16 “Sheria ya Musa na Maandiko ya manabii yalitumiwa mpaka wakati wa Yohana Mbatizaji. Tangu wakati huo Habari Njema za Ufalme wa Mungu zinahubiriwa na kila mtu anafanya bidii kuingia huko. 17 Lakini ni rahisi zaidi kwa mbingu na nchi kutoweka kuliko hata herufi moja katika sheria kufutwa.

18 Mtu ye yote anayempa mke wake talaka na kumwoa mke mwin gine anazini, na mwanamume amwoaye mwanamke aliyeachwa na mumewe, ewe, anazini.”

Mfano Wa Tajiri Na Maskini Lazaro

19 Akasema, “Palikuwa na tajiri mmoja aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, nguo za gharama kubwa, kila siku. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima, alikuwa akiletwa mlangoni kwa huyo tajiri kila siku. 21 Lazaro alikuwa akitamani kula makombo yaliyodondoka mezani kwa tajiri. Hata mbwa walikuwa wakiramba vidonda vyake.

22 “Hatimaye, yule maskini alikufa. Malaika wakamchukua akakae pamoja na Ibrahimu mbinguni. Yule tajiri naye pia akafa, akazikwa. 23 Alipokuwa kuzimuni ambapo alikuwa akiteseka, alita zama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro karibu yake. 24 Akaita, ‘Baba Ibrahimu, nionee huruma umtume Lazaro achovye japo ncha ya kidole chake katika maji aupoze ulimi wangu maana ninateseka kwenye moto huu.’ 25 Lakini Ibrahimu akamjibu, ‘Mwa nangu, kumbuka kwamba ulipokuwa hai ulipata kila kitu kizuri uli chotaka, ambapo Lazaro alipokea mabaya. Lakini sasa anafarijika hapa na wewe unateseka. 26 Isitoshe, kati yetu na ninyi huko, kumewekwa bonde kubwa lisilopitika ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko au kutoka huko kuja huku wasiweze.’ 27 Akasema, ‘Basi, baba, tafadhali umtume Lazaro aende nyumbani kwa baba yangu, 28 awaonye ndugu zangu, wasije wao pia wakaletwa mahali hapa pa mateso watakapokufa.’ 29 Ibrahimu akamjibu, ‘Ndugu zako wanazo sheria za Musa na maandiko ya Manabii. Itawapasa watii hayo.’ Lakini yule tajiri akazidi kumsihi, 30 ‘Hapana baba Ibrahimu, ndugu zangu hawatashawishiwa na hayo. Lakini mtu kutoka kuzimu akitumwa kwao watatubu na kuziacha dhambi zao.’

31 “Ibrahimu akamwambia, ‘Wasiposikiliza na kutii sheria za Musa na Maandiko ya manabii, hawatashawishika kutubu hata kama mtu akifufuka kutoka kuzimu.”’

17 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Majaribu yanayowafanya watu watende dhambi hayana budi kuwepo. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha. Ingekuwa nafuu kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito shingoni na kuzamishwa baharini kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi. Kwa hiyo, jihadharini. Ndugu yako akikukosea mwonye; akiomba msamaha, msamehe. Hata kama akikuko sea mara saba kwa siku na kila mara aje kwako akisema, ‘Nisa mehe

Wanafunzi wakamwambia Bwana, “Tuzidishie imani.” Aka waambia, “Kama mngekuwa na imani kiasi cha punje ndogo sana ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu, ‘Ng’oka na mizizi yote ukaote baharini,’ nao ungewatii!”

Wajibu Wa Mtumishi

“Tuseme mmoja wenu ana mtumishi aliyekwenda shambani kulima au kuchunga kondoo. Je, mtumishi huyo akirudi utamwambia, ‘Karibu keti ule chakula’? Hata kidogo. Badala yake utamwambia, ‘Nitayarishie chakula na ujiandae kunihudumia ninapokula na kunywa, na baada ya hapo unaweza kula chakula chako.’ Wala hutamshukuru mtumishi huyo kwa kutimiza wajibu wake. 10 Hali kadhalika nanyi, baada ya kufanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi ni watumishi tusiostahili, tumetimiza wajibu wetu tu.”’

Yesu Atakasa Wakoma Kumi

11 Yesu alipokuwa akienda Yerusalemu alipitia kati ya Samaria na Galilaya. 12 Alipokuwa akikaribia kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma walikutana naye. 13 Wakasimama mbali wakaita kwa nguvu, “Yesu! Bwana! tuonee huruma!” 14 Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Na walipokuwa wakienda, wakapona ukoma wao. 15 Mmoja wao alipoona kwamba ame pona, akarudi kwa Yesu akimsifu Mungu kwa sauti kuu. 16 Kwa heshima kubwa akajitupa miguuni kwa Yesu akamshukuru. Yeye ali kuwa ni Msamaria .

17 Yesu akauliza, “Hawakuponywa wote kumi? Wako wapi wale tisa wengine? 18 Hakuna hata mmoja aliyekumbuka kurudi kumsifu Mungu isipokuwa huyu mgeni?” 19 Akamwambia, “Inuka, uende; imani yako imekuponya.” Ufalme Wa Mungu Utakavyokuja

20 Siku moja, Mafarisayo walipomwuliza Yesu Ufalme wa Mungu utakuja lini, aliwajibu hivi: “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuone kana, 21 wala watu hawatasema, ‘Huu hapa’ au ‘Ule kule’ kwa maana Ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”

22 Kisha akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona siku yangu moja, mimi Mwana wa Adamu lakini ham taiona. 23 Watu watawaambia, ‘Yule pale’ au, ‘Huyu hapa!’ Msiwa kimbilie. 24 Kwa maana kama umeme unavyomulika mbingu kutoka upande mmoja hadi mwingine, ndivyo itakavyokuwa siku ya kuja kwangu, mimi Mwana wa Adamu. 25 Lakini kwanza itanipasa nite seke sana na kukataliwa na watu wa kizazi hiki. 26 Kama ilivy okuwa nyakati za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa siku ya kurudi kwangu, mimi Mwana wa Adamu. 27 Wakati wa Nuhu watu walikuwa wakila, wakinywa, wakioa na kuolewa mpaka siku ile Nuhu alipoingia katika safina. Ndipo mafuriko yakaja yakawaangamiza wote. 28 Hata nyakati za Lutu ilikuwa hivyo hivyo. Watu walikuwa wakila, waki nywa, wakifanya biashara, wakilima na kujenga. 29 Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, moto ulishuka kutoka mbinguni uka waangamiza wote. 30 Ndivyo itakavyokuwa siku ambapo mimi Mwana wa Adamu nitakapotokea kwa utukufu.

31 “Siku hiyo, mtu akiwa darini na vitu vyake vikiwa ndani, asiteremke kuvichukua. Hali kadhalika atakayekuwa shambani asi rudi nyumbani kuchukua cho chote. 32 Kumbukeni yaliyompata mke wa Lutu! 33 Mtu ye yote anayejaribu kusalimisha maisha yake atayapoteza; na ye yote atakayekuwa tayari kuyapoteza maisha yake atayaokoa. 34 Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa wamelala kitanda kimoja; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa. 35 Wana wake wawili watakuwa wanatwanga pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.” [ 36 Wanaume wawili watakuwa wanafanya kazi pamoja shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.] 37 Wakamwuliza, “Haya yatatokea wapi Bwana?” Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, ndipo tai wanapokutanika.” Mfano Wa Hakimu Dhalimu

Yesu Azungumzia Tena Juu Ya Kifo Chake

18 Yesu akawachukua wale wanafunzi wake kumi na wawili kando akawaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu, na yote yaliy oandikwa na manabii kunihusu mimi Mwana wa Adamu yatatimia. Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. Na alikuwapo mjane mmoja katika mji huo ambaye alikuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, ‘Tafadhali niamulie haki kati yangu na adui yangu.’ Kwa muda mrefu yule hakimu hakufanya lo lote. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, ‘Simwogopi Mungu wala simjali mtu lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbua na kesi yake, nitamwamulia haki asije akanichosha kwa kuja kwake mara kwa mara.”’ Bwana akasema, “Mnasikia asemavyo huyu hakimu dhalimu. Na Mungu je, hatawatendea haki watu wake wanaomlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwapa msaada? Nina waambieni atahakikisha amewatendea haki upesi. Lakini je, mimi Mwana wa Adamu nitakaporudi duniani nitakuta watu wanadumu katika imani?”

Mfano Wa Farisayo Na Mtoza Ushuru

Yesu alitoa mfano huu kwa ajili ya wale waliojiona kuwa wao ni wenye haki na kuwadharau wengine. 10 Watu wawili walikwenda hekaluni kusali, mmoja wao alikuwa Farisayo na mwingine alikuwa mtoza ushuru. 11 yule Farisayo alisimama akasali kimoyomoyo. ‘Ninakushukuru Mungu kwa sababu mimi si kama watu wengine: wany ang’anyi, wadhalimu, wazinzi, au kama huyu mtoza ushuru. 12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma na kutoa sehemu ya kumi ya mapato yangu.’ 13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali. Hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni; bali alijipiga kifuani kwa majuto akasema, ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’

14 Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu na wala si yule Farisayo. Kwa maana ye yote ajikwezaye atashushwa na ye yote ajinyenyekezaye, atainuliwa.”

Yesu Awabariki Watoto Wadogo

15 Watu wakamletea Yesu watoto wao wachanga ili awaguse. Wanafunzi walipowaona, wakawakemea. 16 Lakini Yesu akawaita wale watoto waje kwake, akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa watu walio kama hawa watoto. 17 Nawaambia hakika, ye yote ambaye hataupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.”

18 Kiongozi mmoja akamwuliza Yesu, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

19 Yesu akamjibu, “Mbona unaniita mwema? Hakuna mtu aliye mwema ila Mungu peke yake. 20 Unazifahamu amri: ‘Usizini, usiue, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako?”’ 21 Akajibu, “Amri zote hizi nimezishika tangu utoto wangu.”

22 Yesu aliposikia haya, akamwambia, “Bado unahitaji kufa nya jambo moja. Nenda ukauze vitu vyote ulivyo navyo, uwagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.” 23 Aliposikia hayo alisikitika, kwa maana alikuwa tajiri sana.

24 Yesu alipoona yule kiongozi amesikitika, akasema, “Jinsi gani ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu! 25 Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.” 26 Wale waliosi kia hayo wakauliza, “Kama ni hivyo, ni nani basi awezaye kuoko lewa?” 27 Yesu akajibu, “Yasiyowezekana kwa binadamu yaweze kana kwa Mungu.” 28 Ndipo Petro akasema, “Sisi je? Tumeacha vyote tulivyokuwanavyo tukakufuata!” 29 Yesu akajibu, “Nawaam bia hakika, hakuna hata mmoja aliyeacha nyumba yake, au mke, ndugu, wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, 30 ambaye hatapewa na Mungu mara nyingi zaidi ya hivyo katika maisha haya na kupata uzima wa milele katika maisha yajayo.” 32 Nitatiwa mikononi mwa watawala wa Kirumi. Watu watanizomea, watanitukana na kunitemea mate. 33 Watanipiga na kuniua, lakini siku ya tatu nitafufuka.”

34 Wanafunzi wake hawakuelewa mambo haya. Maana ya maneno haya ilikuwa imefichika kwao, nao hawakujua Yesu alikuwa anazun gumzia nini.

Yesu Amponya Kipofu

35 Yesu na wafuasi wake walipokaribia Yeriko, walimpita kipofu mmoja aliyekuwa amekaa kando ya njia, akiomba fedha. 36 Kipofu huyo aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza, “Kuna nini?” 37 Wakamwambia, “Yesu Mnazareti anapita.” 38 Akaita kwa sauti kuu, “Yesu, Mwana wa Daudi! Nionee huruma!” 39 Wale waliokuwa wakiongoza msafara wakamkemea wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapiga kelele zaidi, “Mwana wa Daudi! Nionee huruma!”

40 Yesu akasimama, akaagiza huyo mtu aletwe kwake. Alipo karibia, Yesu akamwuliza, 41 “Unataka nikufanyie nini?” Aka jibu, “Bwana, nataka kuona.”

42 Yesu akamwambia, “Basi upate kuona; imani yako imekupo nya.” 43 Akaweza kuona mara hiyo hiyo akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walioshuhudia mambo hayo, nao wakamsifu Mungu. 19 Yesu akaingia Yeriko, akiwa safarini kuelekea Yerusalemu. Hapo, alikuwapo mtu mmoja mkuu wa watoza kodi na pia mtu tajiri, jina lake Zakayo. Yeye alitamani sana kumwona Yesu lakini hakuweza kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, naye alikuwa mfupi sana. Kwa hiyo akatangulia mbio mbele ya umati akapanda juu ya mkuyu ili amwone Yesu ambaye angepitia njia ile. Yesu alipofika chini ya huo mkuyu, akatazama juu akamwambia: “Zakayo! Shuka upesi, kwa maana leo nitakuwa mgeni nyumbani kwako!” Mara moja Zakayo akashuka, akamkaribisha Yesu nyumbani kwake kwa furaha kubwa. Watu wote waliokuwepo, wakaanza kunung’unika, “Amekwenda kuwa mgeni nyumbani kwa mwenye dhambi!” Lakini Zakayo akasimama akamwambia Bwana, “Sikia Bwana, nusu ya mali yangu ninaitoa hivi sasa niwagawie maskini, na kama nimemdhulumu mtu ye yote, nitamrudishia mara nne zaidi.” Yesu akamwambia, “Leo, wokovu umeingia nyumba hii, kwa sababu huyu naye ni mtoto wa Ibrahimu. 10 Kwa maana mimi Mwana wa Adamu nimekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.”

Mfano Wa Fedha

11 Wakati walipokuwa wanasikiliza haya, Yesu aliendelea kuwaambia mfano. Wakati huo watu walikuwa wakidhani kwamba kwa kuwa walikuwa wanakaribia Yerusalemu, Ufalme wa Mungu ungetokea mara. 12 Kwa hiyo akawaambia: “Mtu mmoja wa ukoo wa kitawala, alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi. 13 Akawaita watumishi wake kumi akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Zitumieni kufanyia biash ara mpaka nitakaporudi.’ 14 Lakini raia wake walimchukia wakapeleka ujumbe usemao, ‘Hatutaki huyu mtu awe mfalme wetu. ’ 15 Hata hivyo alipewa ufalme akarudi nyumbani. Kisha akawaita wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha, ili afahamu faida kila mmoja wao aliyopata.

16 “Wa kwanza akaja, akasema, ‘Bwana, kutokana na fedha uliyoniachia nimepata faida mara kumi zaidi.’ 17 Yule bwana akamjibu, ‘Umefanya vizuri mtumishi mwema! Kwa sababu umekuwa mwaminifu katika wajibu mdogo sana, nakupa mamlaka juu ya miji kumi.’

18 “Wa pili naye akaja, akasema, ‘Bwana, fedha yako imeleta faida mara tano zaidi.’ 19 Bwana wake akajibu, ‘Nakupa mamlaka juu ya miji mitano.’ 20 Kisha akaja mtumishi mwingine akasema, ‘Bwana hii hapa fedha yako. Niliitunza vizuri kwenye kitambaa. 21 Nilikuogopa, kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unachukua ambapo hukuweka kitu na unavuna mahali ambapo hukupanda kitu.’

22 “Bwana wake akamjibu, ‘Nitakuhukumu kwa maneno yako mwe nyewe, wewe mtumishi mwovu ! Kama ulifahamu kwamba mimi ni mtu mkali, nichukuaye mahali ambapo sikuweka kitu na kuvuna ambapo sikupanda; 23 kwa nini basi hukuweka fedha zangu benki ili nita kaporudi nizichukue na faida yake?’ 24 Ndipo akawaambia wale waliokuwa wamesimama karibu , ‘Mnyang’anyeni fungu lake la fedha mkampe yule mwenye kumi.’ 25 Wakamwambia, ‘Bwana, mbona tayari anayo mafungu kumi’? 26 Akajibu, ‘Nawahakikishieni kwamba, kila aliye na kitu, Mungu atamwongezea; na yule asiyetumia alicho nacho, atanyang’anywa hata hicho alicho nacho. 27 Sasa nileteeni wale maadui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme wao; waleteni hapa muwaue mbele yangu.”’

Yesu Aingia Yerusalemu

28 Alipokwisha kusema haya, Yesu alikaa mbele ya msafara akielekea Yerusalemu. 29 Na alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye mlima wa Mizeituni aliwatuma wanafunzi wawili akawaagiza hivi, 30 “Nendeni katika kijiji kile kilicho mbele yenu. Mtaka pokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana-punda ambaye hajapandwa na mtu bado, amefungwa. Mfungueni, mumlete hapa. 31 Kama mtu akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji.”’

32 Wale waliotumwa wakaenda, wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaambia. 33 Walipokuwa wanamfungua yule mwana- punda wenyewe wakawauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwana-punda?” 34 Wale wanafunzi wakajibu, “Bwana anamhitaji.” 35 Wakamleta kwa Yesu. Wakatandika mavazi yao juu ya huyo mwana-punda, kisha wakampandisha Yesu juu yake. 36 Alipokuwa akienda, watu wakatan daza nguo zao barabarani. 37 Alipokaribia mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote wa wanafunzi wake wakaanza kwa sauti kuu kumsifu Mungu kwa furaha kwa ajili ya miujiza yote waliyoiona Yesu akifanya, 38 wakasema: “Amebarikiwa Mfalme anayekuja kwa jina la Bwana! Amani mbinguni na Utukufu kwa Mungu.” 39 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwemo katika umati wakamwambia, “Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako.” 40 Yesu akawajibu, “Nawaambia, hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele.”

Yesu Anaulilia Mji Wa Yerusalemu

41 Alipokaribia Yerusalemu, akauona mji, aliulilia,

42 akasema, “Laiti ungalijua leo jinsi ya kupata amani! Lakini sasa huoni! 43 Kuna siku ambapo maadui zako watakuzungushia ukuta na kukuzingira na kukushambulia kutoka kila upande. 44 Watakutupa chini wewe na wanao ndani ya kuta zako na hawataacha hata jiwe moja juu ya jingine. Hii ni kwa sababu hukutaka kutambua wakati

Yesu Aingia Hekaluni

45 Ndipo akaingia Hekaluni akaanza kuwafukuza wale wal iokuwa wakifanya biashara humo. 46 Akawaambia, “Imeandikwa katika Maandiko, ‘Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala.’ Lakini ninyi mmeigeuza kuwa pango la wanyang’anyi.”

47 Kila siku alikuwa akifundisha Hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakiungwa mkono na viongozi wengine walijaribu kila njia wapate kumwua 48 lakini hawakupata nafasi kwa sababu watu wote waliomfuata waliyasikiliza maneno yake kwa makini na kuyazingatia. Yesu Aulizwa Kuhusu Mamlaka Yake

20 Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, wakuu wa makuhani, walimu wa sheria na wazee walifika Hekaluni wakamwuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?”

Akawajibu, “Na mimi nitawauliza swali. Je, mamlaka ya Yohana ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au kwa wanadamu? ” Wakaanza kubishana wao kwa wao wakisema, “Tukisema, ‘Kwa Mungu’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ Na tukisema ‘Kwa wana damu,’ watu wote watatupiga mawe kwa sababu wanaamini kabisa kwamba Yohana alikuwa nabii.” Basi wakajibu, “Hatujui mamlaka yake yalitoka wapi.” Yesu akawaambia, “Na mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.’ ’

Mfano Wa Shamba La Mizabibu Na Wakulima

Akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alipanda mizabibu katika shamba lake, akalikodisha kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwa muda mrefu. 10 Wakati wa mavuno akamtuma mtumishi kwa hao wakulima aliowakodisha shamba ili wampatie sehemu ya mavuno. Lakini wale wakulima wakampiga na kumfukuza mikono mitupu. 11 Akamtuma mtumishi mwingine; naye pia wakam piga, wakamfanyia mambo ya aibu na kumfukuza. 12 Akampeleka wa tatu; wakamjeruhi na kumtupa nje ya shamba.

13 “Basi yule mwenye shamba la mizabibu akasema, ‘Nifanye nini? Nitamtuma mwanangu nimpendaye, bila shaka yeye watamhesh imu.’ 14 Lakini wale wakulima walipomwona, wakashauriana, ‘Huyu ndiye mrithi, hebu tumwue ili sisi turithi hili shamba.’ 15 Kwa hiyo wakamtoa nje ya shamba, wakamwua.” Ndipo Yesu akauliza, “Sasa yule mwenye shamba atawafanyia nini wakulima hawa?

16 Atakuja awaue awapatie watu wengine shamba hilo.” Watu waliposikia hayo wakasema, “Jambo hili lisi tokee!”

17 Lakini Yesu akawakazia macho akasema, “Basi ni nini maana ya maandiko haya, ‘Lile jiwe walilokataa waashi limekuwa jiwe la msingi.’

18 “Kila aangukaye kwenye jiwe hilo atakatika vipande vipande, na ye yote ambaye litamwangukia atasagika sagika.”

19 Waalimu wa sheria na wakuu wa makuhani wakatafuta njia ya kumkamata mara moja kwa sababu walifahamu kwamba huo mfano aliou toa uliwahusu wao. Lakini waliwaogopa watu.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica