Bible in 90 Days
Kuhusu Kulipa Kodi
20 Kwa hiyo wakawa wanamvizia. Wakawatuma wapelelezi wal iojifanya kuwa wana nia njema ya kujifunza. Walitumaini kumtega kwa maswali ili wamkamate kwa lo lote atakalosema, walitumie kumshtaki kwa Gavana. 21 Wale wapelelezi wakamwuliza, “Mwalimu, tunajua kwamba maneno yako na mafundisho yako ni ya haki, kwamba huna upendeleo, na kwamba unafundisha njia ya Mungu kwa kweli. 22 Je, sheria ya Musa inaturuhusu au haituruhusu kulipa kodi kwa
Kaisari?”
23 Lakini Yesu akatambua kwamba wanamtega, kwa hiyo akawaam bia, 24 “Nionyesheni sarafu ya fedha. Je, picha hii na maand ishi haya ni ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” 25 Aka waambia, “Basi, mpeni Kaisari vilivyo vyake na mpeni Mungu vil ivyo vyake.” 26 Wakashindwa kumkamata kwa maneno aliyosema mbele ya watu. Jibu lake liliwashangaza mno, wakakosa la kusema. Yesu Afundisha Kuhusu Ufufuo
27 Baadhi ya Masadukayo , wale wanaosema kwamba hakuna ufu fuo wa wafu, wakamjia Yesu wakamwuliza, 28 “Mwalimu, katika sheria ya Musa , tunasoma kwamba kama mtu akifariki akamwacha mkewe bila mtoto, basi kaka yake amwoe huyo mjane ili amzalie marehemu watoto. 29 Walikuwepo ndugu saba. Wa kwanza akafa bila kuzaa mtoto. 30 Kaka wa pili akamwoa huyo mjane 31 na wa tatu pia. Ikawa hivyo mpaka ndugu wote saba wakawa wamemwoa huyo mama na wote wakafa pasipo kupata mtoto. 32 Mwishowe mama huyo naye akafa. 33 Je, siku ya ufufuo, mwanamke huyo ambaye aliolewa na wote saba atahesabiwa kuwa ni mke wa nani?”
34 Yesu akawajibu , “Katika maisha haya watu huoa na kuol ewa, 35 lakini wale ambao Mungu atawaona wanastahili kufufuka kutoka kwa wafu, watakapofika mbinguni hawataoa au kuolewa. 36 Hawa hawawezi kufa tena kwa sababu wao ni kama malaika; wao ni wana wa Mungu kwa kuwa wamefufuka kutoka kwa wafu. 37 Hata Musa alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka. Alimwita Bwana, ‘Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo,’ wakati Mungu aliposema naye katika kile kichaka kilichokuwa kikiwaka bila kuungua. 38 Yeye ni Mungu wa watu walio hai na si Mungu wa wafu kwa sababu kwa Mungu watu wote ni hai.” 39 Baadhi ya walimu wa sheria wakasema, “Mwalimu, umesema sawa kabisa!” 40 Na hakuna mtu aliyethubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.
Uhusiano Kati Ya Kristo Na Daudi
41 Kisha akawaambia, “Inakuwaje watu wanasema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? 42 Maana Daudi mwenyewe katika kitabu cha Zaburi anasema, ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: kaa kulia kwangu 43 mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’
44 Sasa ikiwa Daudi anamwita Kristo ‘Bwana
Yesu Aonya Kuhusu Walimu Wa Sheria
45 Watu wote walipokuwa wakimsikiliza, Yesu akawaambia wana funzi wake, 46 “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa kanzu ndefu na kuamkiwa kwa heshima maso koni. Wao huchagua viti vya mbele katika masinagogi na kukaa kwe nye sehemu za wageni rasmi katika sherehe. 47 Wanawadhulumu wajane mali zao na kisha wanasali sala ndefu ili waonekane wao ni watu wema. Mungu atawaadhibu vikali zaidi kwa ajili ya haya.” Sadaka Ya Mjane
21 Alipokuwa Hekaluni Yesu aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la sadaka. 2 Akamwona na mama mmoja mjane, maskini sana, akiweka humo sarafu mbili. 3 Akasema, “Nawaambia kweli, huyu mjane ametoa sadaka kubwa zaidi kuliko hao wengine wote. 4 Kwa maana hao wengine wametoa sehemu ndogo tu ya utajiri wao, lakini yeye, ingawa ni maskini, ametoa vyote alivyokuwa navyo.”
Dalili Za Siku Za Mwisho
5 Baadhi ya watu walikuwa wakizungumza kuhusu Hekalu jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na mapambo maridadi yaliyotolewa kama sadaka kwa Mungu. Yesu akawaambia, 6 “Wakati unakuja ambapo vyote hivyo mnavyovistaajabia sasa vitabomolewa, halitabaki hata jiwe moja juu ya jingine.” 7 Wakamwuliza, “Mwalimu, mambo haya yatatokea lini na ni dalili gani zitaonyesha kwamba yanakari bia?” 8 Akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja wakitumia jina langu, na kusema, ‘Mimi ndiye’ na ‘Wakati umekaribia’. Msiwafuate. 9 Na mtakaposikia habari za vita na machafuko, msiogope, kwa maana hayo ni lazima yatokee kwanza, ila mwisho hautatokea wakati huo.”
10 Kisha akawaambia: “Taifa moja litapigana na taifa lin gine na utawala mmoja utapigana na utawala mwingine. 11 Kutaku wepo na matetemeko ya ardhi, njaa kali na magonjwa ya kuambukiza katika sehemu mbalimbali; kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.”
Mateso
12 “Lakini kabla haya yote hayajatokea watu watawakamata ninyi na kuwatesa. Mtashtakiwa mbele ya wakuu wa masinagogi na kufungwa magerezani; na wengine mtapelekwa kushtakiwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jina langu. 13 Na hii itawapa nafasi ya kutoa ushuhuda kuhusu imani yenu. 14 Lakini msiwe na wasiwasi juu ya matayarisho ya utetezi wenu kabla ya mashtaka. 15 Kwa maana nitawapa maneno na hekima ambayo maadui zenu hawa taweza kukataa au kupinga. 16 Mtasalitiwa na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na baadhi yenu mtauawa. 17 Watu wote watawa chukia kwa ajili yangu. 18 Lakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu! 19 Simameni imara nanyi mtaokoa nafsi zenu.”
Kuteketezwa Kwa Yerusalemu
20 “Mkiona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, faham uni kwamba karibu utaangamizwa. 21 Wakati huo, wale walio Yudea wakimbilie milimani; walio mjini Yerusalemu waondoke humo na wale walioko mashambani wasije mjini. 22 Kwa sababu huu utakuwa wakati wa kulipiza kisasi ili yale yote yaliyosemwa kwenye Maan diko yatimie.
23 “Ole wao akina mama watakaokuwa waja wazito na wata kaokuwa wakinyonyesha! Kutakuwa na dhiki nchini na ghadhabu ya Mungu itakuwa juu ya watu wa taifa hili. 24 Wengine watauawa kwa silaha na wengine watachukuliwa mateka na kupelekwa nchi mbalim bali. Na Yerusalemu itamilikiwa na watu wa mataifa mengine mpaka muda wa mataifa hayo utakapokwisha.”
Kuja Kwa Mwana Wa Adamu
25 “Kutakuwa na matukio ya ajabu kwenye jua, mwezi na nyota. Hapa ulimwenguni, mataifa yatakuwa katika dhiki na wasi wasi kutokana na ngurumo na dhoruba za kutisha zitakazotokea baharini. 26 Watu watakufa moyo kwa hofu na wasiwasi kuhusu yale wanayoogopa kuwa yataukumba ulimwengu; kwani nguvu za anga zita tikisika. 27 Ndipo wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika wingu kwa uwezo na utukufu mkuu. 28 Mambo haya yakianza kutokea, simameni imara, mjipe moyo, kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.”
29 Akawaambia mfano, “Utazameni mtini na miti mingine yote. 30 Inapochipua majani, mnatambua ya kuwa wakati wa mavuno uko karibu. 31 Hali kadhalika, mkiyaona mambo haya yanatokea, faham uni kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia. 32 Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitakwisha kabla mambo haya hayajatokea. 33 Mbingu na nchi zitatoweka lakini maneno yangu yatadumu daima.” Siku Ya Mwisho Itakuja Ghafla
34 Jihadharini msije mkatawaliwa na ulafi, ulevi na wasiwasi wa maisha haya. Kisha siku ikafika pasipo ninyi kutazamia mka naswa! 35 Kwa maana siku hiyo itawakumba watu wote waishio duniani. 36 Kaeni macho na ombeni ili Mungu awawezeshe kuepuka yale yote yatakayotokea na mweze kusimama mbele yangu mimi Mwana wa Adamu.”
37 Kila siku Yesu alikuwa akifundisha Hekaluni na jioni ili pofika alikwenda kulala kwenye mlima wa Mizeituni. 38 Na asubuhi na mapema watu wote walikuwa wakija Hekaluni kumsikiliza.
22 Sikukuu ya Mikate isiyotiwa Chachu, iitwayo Pasaka, ili kuwa imekaribia. 2 Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakawa wanatafuta njia ya kumwua Yesu kwa siri kwa sababu waliwaogopa watu.
3 Shetani akamwingia Yuda aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili. 4 Yuda akaenda kwa makuhani wakuu na wakubwa wa walinzi wa Hekalu akawaeleza jinsi ambavyo angeweza kumsaliti Yesu. 5 Wakafurahi na wakaahidi kumlipa fedha. 6 Naye akaridhika, akaanza kutafuta nafasi nzuri ya kumsaliti Yesu kwa siri. Maandalizi Ya Chakula Cha Pasaka
7 Ikafika siku ya Mikate isiyotiwa Chachu. Siku hiyo Mwana- Kondoo wa Pasaka huchinjwa. 8 Yesu akawatuma Petro na Yohana, akawaagiza, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka.” 9 Wakam wuliza, “Tukaandae wapi?” 10 Akawajibu, “Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mwanaume aliyebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka kwenye nyumba atakayoingia, 11 kisha mwambieni mwenye nyumba, Mwalimu anauliza, kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka? 12 Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani ambacho kina fanicha zote. Fanyeni maandalizi humo.”
13 Wakaenda wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaam bia. Kwa hiyo wakaandaa chakula cha Pasaka.
14 Wakati ulipofika Yesu akaketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 15 Kisha akawaambia “Nimetamani mno kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. 16 Kwa maana, nawaambieni, hii ni mara yangu ya mwisho kula Pasaka mpaka maana halisi ya Pasaka itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu.” 17 Akapokea kikombe cha divai akashukuru, akasema, “Chukueni mnywe wote. 18 Kwa maana, nawaambieni, tangu sasa sitakunywa tena divai hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.”
19 Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.” 20 Vivyo hivyo baada ya kula, aka chukua kile kikombe cha divai akasema, “Hiki kikombe ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu. 21 Lakini huyo atakayenisaliti amekaa nasi hapa mezani kama rafiki. 22 Mimi Mwana wa Adamu sina budi kufa kama ilivyokusudiwa na Mungu, lakini ole wake huyo mtu atakayenisaliti.” 23 Wakaanza kuulizana wao kwa wao ni nani kati yao angefanya kitu kama hicho.
Ubishi Kuhusu Ukubwa
24 Pia ukazuka ubishi kati ya wanafunzi kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa kati yao. 25 Yesu akawaambia, “Wafalme wa dunia huwatawala watu wao kwa mabavu na wenye mam laka huitwa ‘Wafadhili.’ 26 Ninyi msifanye hivyo. Aliye mkubwa wenu awe kama ndiye mdogo kabisa; na kiongozi wenu awe kama mtum ishi. 27 Kwani mkubwa ni nani? Yule aketiye mezani au yule anayemhudumia? Bila shaka ni yule aliyekaa mezani. Lakini mimi niko pamoja nanyi kama mtumishi wenu.
28 “Ninyi mmekuwa pamoja nami katika majaribu yangu: 29 na kama Baba yangu alivyonipa mamlaka ya kutawala; mimi nami nina wapa ninyi mamlaka hayo hayo. 30 Mtakula na kunywa katika karamu ya Ufalme wangu na kukaa katika viti vya enzi mkitawala makabila kumi na mawili ya Israeli.”
Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana
31 Yesu akasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, shetani ameomba ruhusa kwa Mungu awapepete ninyi kama ngano. 32 Lakini nimekuombea wewe ili imani yako isipotee. Na utakaponirudia mimi, uwatie moyo ndugu zako.”
33 Petro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda nawe gerezani na hata kufa.” 34 Yesu akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika leo usiku, utakana mara tatu kwamba hunijui.”
Kujiandaa Wakati Wa Hatari
35 Kisha Yesu akawauliza, “Nilipowatuma mwende bila mfuko, wala mkoba wala viatu, mlipungukiwa na kitu?” Wakajibu, “La.” 36 Akawaambia, “Lakini sasa, aliye na mfuko au mkoba auchukue. Asiye na upanga, auze koti lake anunue upanga. 37 Kwa sababu, nawambieni, yale Maandiko yaliyosema kwamba ‘Alihesabiwa pamoja na wahalifu’ yananihusu mimi na hayana budi kutimizwa. Naam, yale yaliyoandikwa kunihusu mimi yanatimia.” 38 Wakamwambia, “Bwana, tazama hapa kuna mapanga mawili.” Akawajibu, “Inatosha!. Yesu Asali Kwenye Mlima Wa Mizeituni
39 Ndipo Yesu akaondoka kuelekea kwenye mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa kawaida yake, na wanafunzi wake wakamfuata. 40 Alipofika huko akawaambia wanafunzi, “Ombeni kwamba msiingie katika majaribu.” 41 Akaenda mbali kidogo nao, kama umbali anaoweza mtu kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba 42 akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki cha mateso. Lakini si kwa mapenzi yangu, bali mapenzi yako yafanyike.” [ 43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. 44 Na alipokuwa katika uchungu mkubwa, akaomba kwa bidii zaidi na jasho lake likawa kama matone ya damu ikidondoka ardhini.] 45 Baada ya kuomba, akawarudia wanafunzi wake akawakuta wamelala, wamechoka kwa huzuni. 46 Akawauliza, “Mbona mnalala? Amkeni muombe ili msiingie katika majaribu.”
Yesu Akamatwa
47 Wakati Yesu alipokuwa bado anazungumza, pakatokea kundi la watu likiongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wana funzi kumi na wawili. Akamsogelea Yesu ili ambusu. 48 Lakini Yesu akamwuliza, “Yuda! Unanisaliti mimi Mwana wa Adamu kwa busu?” 49 Wafuasi wa Yesu walipoona yanayotokea, wakasema, “Bwana, tutumie mapanga yetu?” 50 Na mmoja wao akampiga mtum ishi wa kuhani mkuu kwa panga, akamkata sikio la kulia. 51 Lakini Yesu akasema, “Acheni!” Akaligusa sikio la yule mtu, akamponya. 52 Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu na wakuu wa walinzi wa Hekalu na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mme kuja na mapanga na marungu, kana kwamba mimi ni jambazi? 53 Kila siku nilikuwa pamoja nanyi lakini hamkunikamata. Lakini wakati huu, ambapo mtawala wa giza anafanya kazi, ndiyo saa yenu.”
Petro Amkana Yesu
54 Wakamkamata Yesu, wakamchukua wakaenda naye nyumbani kwa kuhani mkuu. Petro akawafuata kwa mbali. 55 Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, na Petro akaketi na wale waliokuwa wakiota moto. 56 Msichana mmoja mfanyakazi akamwona Petro ameketi karibu na moto. Akamwangalia kwa makini, kisha akasema, “Huyu mtu pia ali kuwa pamoja na Yesu!” 57 Lakini Petro akakana akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!” 58 Baadaye kidogo mtu mwingine akamwona Petro, akasema, “Wewe pia ni mmoja wao.” Petro akajibu, “Bwana, mimi si mmoja wao!” 59 Baada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akasisitiza, “Kwa hakika huyu mtu alikuwa na Yesu, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.” 60 Petro akajibu, “Mimi sijui unalosema!” Na wakati huo huo, akiwa bado anazun gumza, jogoo akawika. 61 Yesu akageuka akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka yale maneno ambayo Bwana alimwambia, “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.” 62 Akaenda nje, akalia kwa uchungu . Yesu Achekwa Na Kupigwa
63 Watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. 64 Wakamfunga kitambaa usoni kisha wakasema, “Hebu nabii tuambie! Ni nani amekupiga?” 65 Wakamwambia maneno mengi ya kumtukana. Yesu Apelekwa Mbele Ya Baraza
66 Kulipokucha, Baraza la wazee wa Wayahudi, makuhani wakuu na walimu wa sheria wakakutana. Yesu akaletwa mbele yao. 67 Wakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo, tuambie.” Yesu akawa jibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini, 68 na nikiwauliza swali, hamtanijibu. 69 Lakini hivi karibuni, mimi Mwana wa Adamu nita kaa upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi.” 70 Wote wakasema, “Ndio kusema wewe ndiye Mwana wa Mungu?” Akawajibu, “Ninyi ndio mmesema kwamba Mimi ndiye.” 71 Kisha wakasema, “Kwa nini tutafute ushahidi zaidi? Sisi wenyewe tumesikia maneno aliy osema.” Yesu Apelekwa Kwa Pilato
23 Wote waliokuwepo katika Baraza wakasimama, wakampeleka Yesu kwa Pilato. 2 Wakafungua mashtaka yao kwa kusema: “Tumem wona huyu mtu akipotosha taifa letu. Yeye anawaambia watu wasi lipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo, mfalme.” 3 Basi Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamjibu, “Ni kama ulivyosema.” 4 Pilato akawaambia maku hani wakuu na watu wote waliokuwapo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki huyu mtu!” 5 Lakini wao wakakazana kusema, “Anawa chochea watu kwa mafundisho yake katika Yudea yote. Alianzia huko
Yesu Apelekwa Kwa Herode
6 Pilato aliposikia hayo akauliza, ‘Huyu mtu ni Mgalilaya?” 7 Alipofahamu kwamba Yesu alitoka katika mkoa unaotawaliwa na Herode, akampeleka kwa Herode ambaye wakati huo alikuwa Yerus alemu. 8 Herode alifurahi sana kumwona Yesu. Alikuwa amesikia habari zake na kwa muda mrefu akatamani sana kumwona; na pia alitegemea kumwona Yesu akifanya mwujiza. 9 Kwa hiyo akamwuliza Yesu maswali mengi, lakini yeye hakumjibu neno. 10 Wakati huo, makuhani wakuu na walimu wa sheria walikuwepo wakitoa mashtaka yao kwa nguvu sana. 11 Herode na maaskari wake wakamkashifu Yesu na kumzomea. Wakamvika vazi la kifahari, wakamrudisha kwa Pilato. 12 Siku hiyo, Herode na Pilato, ambao kabla ya hapo walikuwa maadui, wakawa marafiki.
Yesu Ahukumiwa Kifo
13 Pilato akawaita makuhani wakuu, viongozi na watu 14 aka waambia, “Mmemleta huyu mtu kwangu mkamshtaki kuwa anataka kuwa potosha watu. Nimemhoji mbele yenu, na sikuona kuwa ana hatia kutokana na mashtaka mliyoleta. 15 Hata Herode hakumwona na kosa lo lote; ndio sababu amemrudisha kwetu. Kama mnavyoona, mtu huyu hakufanya jambo lo lote linalostahili adhabu ya kifo. 16 Kwa hiyo nitaamuru apigwe viboko, kisha nimwachilie.” [ 17 Kwa kawaida, kila sikukuu ya Pasaka ilimlazimu Pilato kuwafungulia mfungwa mmoja].
18 Watu wote wakapiga kelele kwa pamoja, “ Auawe huyo! Tufungulie Baraba!” 19 Baraba alikuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika fujo na mauaji yaliyotokea mjini. 20 Pilato ali taka sana kumwachilia Yesu kwa hiyo akasema nao tena. 21 Lakini wao wakazidi kupiga kelele, “Msulubishe! Msulubishe!” 22 Kwa mara ya tatu Pilato akasema nao tena, “Amefanya kosa gani huyu mtu? Sioni sababu yo yote ya kutosha kumhukumu adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe viboko kisha nimwachilie .”
23 Lakini watu wakazidi kupiga kelele kwa nguvu na kusisi tiza kwamba Yesu asulubiwe. Hatimaye, kelele zao zikashinda. 24 Pilato akaamua kutoa hukumu waliyoitaka. 25 Akamwachia huru yule mtu aliyekuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika fujo na mauaji yaliyotokea mjini; akamkabidhi Yesu mikononi mwao, wamfa nyie watakavyo. Yesu Asulubiwa Msalabani
26 Na walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja ait waye Simoni wa Kirene aliyekuwa anatoka mashambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha atembee nyuma ya Yesu. 27 Umati mkubwa wa watu wakamfuata Yesu ikiwa ni pamoja na wanawake waliokuwa wakimlilia na kuomboleza. 28 Lakini Yesu akawageukia, akawaam bia, “Enyi akina mama wa Yerusalemu, msinililie mimi bali jilil ieni ninyi wenyewe na watoto wenu. 29 Kwa maana wakati utafika ambapo mtasema, ‘Wamebarikiwa akina mama tasa, ambao hawakuzaa na matiti yao hayakunyonyesha.’ 30 Na watu wataiambia milima, ‘Tuangukieni’ na vilima, ‘Tufunikeni’. 31 Kwa maana kama watu wanafanya mambo haya wakati mti ni mbichi, itakuwaje utakapo kauka?”
32 Wahalifu wengine wawili pia walipelekwa wakasulubiwe pamoja na Yesu. 33 Walipofika mahali paitwapo “Fuvu la kichwa,” wakamsulubisha Yesu hapo pamoja na hao wahalifu; mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.
34 Yesu akasema, “Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui wali tendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura. 35 Watu wakasi mama pale wakimwangalia. Viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Si aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama kweli yeye ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.” 36 Askari nao wakam wendea, wakamdhihaki. Wakamletea siki anywe, 37 wakamwambia, “Kama wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe tuone.”
38 Na maandishi haya yaliwekwa kwenye msalaba juu ya kichwa chake: “HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.” 39 Mmoja kati ya wale wahalifu waliosulubiwa naye akamtu kana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe na utuokoe na sisi.”
40 Yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akisema, “Wewe humwogopi hata Mungu! Wote tumehukumiwa adhabu sawa. 41 Adhabu yetu ni ya haki kwa sababu tunaadhibiwa kwa makosa tuliyofanya. Lakini huyu hakufanya kosa lo lote.” 42 Kisha akasema, “Bwana Yesu unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.” 43 Yesu akam jibu, “Nakuambia kweli, leo hii utakuwa pamoja nami peponi.”
Yesu Afa Msalabani
44 Ilikuwa kama saa sita mchana. Kukawa na giza nchi nzima mpaka saa tisa, 45 kwa maana jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likapasuka katikati kukawa na vipande viwili. 46 Yesu akapaza sauti akasema, “Baba, mikononi mwako ninaikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.
47 Mkuu wa maaskari alipoona yaliyotokea, akamsifu Mungu akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.” 48 Na watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hilo walipoy aona hayo, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni.
49 Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wanawake wal iokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyata zama mambo haya. Yesu Azikwa Kaburini
50 Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yusufu mwenyeji wa mji wa Arimathaya, ambaye alikuwa anautazamia Ufalme wa Mungu. Yeye ali kuwa mjumbe wa Baraza na pia alikuwa mtu mwema na mwenye kuheshi mika. 51 Lakini yeye hakukubaliana na wajumbe wenzake katika uamuzi wao na kitendo cha kumsulubisha Yesu. 52 Basi, Yusufu alikwenda kwa Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu. 53 Akaushusha kutoka msalabani, akauzungushia sanda, akauhifadhi katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kaburi hilo lilikuwa halijatumika bado. 54 Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, Siku ya Maandalizi, na sabato ilikuwa karibu ianze. 55 Wale wanawake waliokuwa wamefuatana na Yesu kutoka Galilaya wakamfuata Yusufu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Yesu ulivyolazwa humo. 56 Kisha wakarudi nyumbani wakaandaa marashi na manukato ya kuupaka huo mwili. Lakini waka pumzika siku ya sabato kama ilivyoamriwa.
24 Siku ya Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake wali chukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa wakaenda kaburini. 2 Wakakuta jiwe limeondolewa kwenye mlango wa kaburi. 3 Lakini walipoingia ndani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu. 4 Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hilo, ghafla, watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa sana, wakasimama karibu nao. 5 Wale wanawake, kwa hofu, wakainamisha nyuso zao chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai mahali pa wafu? 6 Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa Gali laya, 7 kwamba ilikuwa lazima Mwana wa Adamu awekwe mikononi mwa watu waovu, asulubiwe na siku ya tatu afufuke.” 8 Wakayakumbuka maneno ya Yesu. 9 Waliporudi kutoka huko kaburini wakaeleza mambo haya kwa wale wanafunzi kumi na mmoja pamoja na wengine wote. 10 Hao wanawake walikuwa ni Mariamu Magdalene, Yoana na Mariamu mama yake Yakobo pamoja na wengine waliofuatana nao. 11 Maelezo yao yalionekana kama upuuzi kwa hiyo hawakuwaamini. 12 Bali Petro akaondoka mbio, akaenda kaburini. Alipoinama, akaiona ile sanda, ila hakuona kitu kingine zaidi. Akarudi nyumbani akis taajabia yaliyotokea.
Yesu Awatokea Wanafunzi Wawili
13 Siku hiyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa wanak wenda kijiji cha Emau, yapata maili saba kutoka Yerusalemu, 14 nao walikuwa wakizungumzia mambo yote yaliyotokea. 15 Wali pokuwa wakizungumza, Yesu mwenyewe alikuja akatembea pamoja nao, 16 lakini wao hawakumtambua. 17 Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumzia wakati mnatembea?” Wakasimama , nyuso zao zikionyesha huzuni. 18 Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamwambia, “Nadhani ni wewe tu katika watu wote wanaoishi Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotokea siku hizi chache zilizopita.”
19 Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu “Mambo yaliyompata Yesu Mnazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele za wanadamu. 20 Makuhani wakuu na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa na wakamsulubisha. 21 Na sisi tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angeliikomboa Israeli. Zaidi ya hayo leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee. 22 Isitoshe, baadhi ya wanawake katika kundi letu wametushtua; walikwenda kaburini leo alfajiri 23 lakini hawakuukuta mwili wake. Waliporudi walisema wamewaona malaika ambao waliwaambia kwamba Yesu yu hai. 24 Baadhi yetu walikwenda kaburini wakakuta mambo ni kama walivyoelezea wale wanawake, ila yeye mwenyewe hawakumwona.”
25 Kisha Yesu akawaambia, “Ninyi ni watu wajinga. Mbona mnaona ugumu kuamini mambo yote yaliyosemwa na Manabii? 26 Je, haikumpasa Kristo kuteswa na kwa njia hiyo aingie katika utukufu wake?” 27 Akawafafanulia maandiko yalivyosema kumhusu yeye, akianzia na maandiko ya Musa na kupitia maandiko yote ya manabii.
28 Walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea na safari. 29 Lakini wakamsihi akae nao wakisema, “Kaa hapa nasi kwa maana sasa ni jioni na usiku unain gia.” Basi akaingia ndani kukaa nao. 30 Alipokuwa nao mezani, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia. 31 Ndipo macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua! Lakini akatoweka, hawakumwona tena.
32 Wakaulizana, “Je, mioyo yetu haikuchangamka kwa furaha alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?” 33 Wakaondoka mara moja, wakarudi Yerusalemu. Wakawakuta wale wanafunzi kumi na mmoja na wale waliokuwa pamoja nao, wamekusany ika 34 wakisema, “Ni kweli Bwana amefufuka! Amemtokea Simoni.” 35 Kisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotokea njiani na jinsi walivyomtambua Yesu alipoumega mkate. Yesu Awatokea Wanafunzi Wake
36 Wakati walipokuwa wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasi mama katikati yao akawasalimu, “Amani iwe nanyi.”
37 Wakashtuka na kuogopa wakidhani wameona mzimu. 38 Lakini akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna mashaka mioyoni mwenu? 39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu mwone kuwa ni mimi. Niguseni mwone. Mzimu hana nyama na mifupa kama mnion avyo.” 40 Aliposema haya aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. 41 Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula cho chote hapa?” 42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa, 43 akakichukua akakila mbele yao.
44 Akawaambia, “Haya ndiyo mambo niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi; kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika she ria ya Musa, katika Maandiko ya manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.” 45 Akawapa uwezo wa kuyaelewa Maandiko, 46 aka waambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. 47 Habari hii ya wokovu itatan gazwa kwanza Yerusalemu hadi kwa mataifa yote, kwamba: kuna msa maha wa dhambi kwa wote watakaotubu na kunigeukia mimi. 48 Ninyi ni mashahidi wa mambo haya. 49 Na sasa nitawapelekea Roho Mtaka tifu kama alivyoahidi Baba yangu; lakini kaeni humu Yerusalemu mpaka mtakapopewa nguvu ya Roho Mtakatifu kutoka mbinguni.”
Yesu Apaa Mbinguni
50 Kisha akawaongoza nje ya mji mpaka Bethania, akainua mikono yake, akawabariki. 51 Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni. 52 Wakamwabudu na kisha wakarudi Yerus alemu wamejawa na furaha;
Neno Alifanyika Mwili
1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watu. 5 Nuru hiyo huangaza gizani na giza haliwezi kamwe kuizima.
6 Mtu mmoja aitwaye Yohana alitumwa na Mungu 7 awaambie watu kuhusu hiyo nuru, ili kwa ushuhuda wake wapate kuamini. 8 Yohana mwenyewe hakuwa ile nuru. Yeye alitumwa kuishuhudia hiyo nuru. 9 Nuru halisi ambayo inawaangazia watu wote ilikuwa inakuja ulim wenguni. 10 Neno alikuwepo ulimwenguni, lakini japokuwa aliumba ulimwengu, watu wa ulimwengu hawakumtambua! 11 Alikuja nyumbani kwake, lakini watu wake hawakumpokea! 12 Bali wote waliompokea na kumwamini aliwapa haki ya kufanywa watoto wa Mungu. 13 Hawa hawakuwa watoto wa Mungu kwa kuzaliwa kwa njia ya asili, wala kwa mapenzi au mipango ya watu bali wamezaliwa na Mungu mwenyewe.
14 Neno akawa mwanadamu akaishi kati yetu akiwa amejaa utu kufu na kweli. Tuliona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee wa Baba. 15 Yohana alishuhudia habari zake, akatangaza: “Huyu ndiye yule niliyewaambia kuwa, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa kuwa alikuwapo kabla sijazaliwa.”’ 16 Na kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema tele. 17 Musa alitule tea sheria kutoka kwa Mungu, lakini Yesu Kristo ametuletea neema na kweli. 18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Lakini Mwanae pekee, ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Baba yake, amemdhihirisha Mungu kwetu.
Ujumbe Wa Yohana Mbatizaji
19 Viongozi wa Wayahudi waliwatuma makuhani na Walawi wakam wulize Yohana, “Wewe ni nani?” 20 Yohana akawajibu wazi wazi pasipo kuficha, “Mimi siye Kristo.” 21 Wakamwuliza, “Wewe ni nani basi? Wewe ni Eliya ?” Akajibu, “Hapana, mimi siye.” “Wewe ni yule Nabii?” Akajibu, “Hapana.” 22 Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Tueleze, wewe hasa ni nani?”
23 Akawajibu kwa kutumia maneno ya nabii Isaya, “Mimi ni sauti ya mtu anayeita kwa sauti kuu nyikani, ‘Nyoosheni njia ata kayopita Bwana.”’ 24 Baadhi ya wale waliotumwa na Mafarisayo 25 walimwuliza, “Kama wewe si Kristo, wala Eliya na wala si yule Nabii, kwa nini unabatiza watu?”
26 Yohana akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji, lakini kati yenu yupo mtu msiyemjua. 27 Yeye anakuja baada yangu, lakini mimi sistahili hata kumvua viatu vyake.”
28 Mambo haya yalitokea Bethania, kijiji kilichoko ng’ambo mashariki ya mto wa Yordani, ambapo Yohana alikuwa akibatiza watu.
Mwana Kondoo Wa Mungu
29 Kesho yake Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, “Tazameni! Huyu ndiye Mwana-Kondoo wa Mungu anayeondoa dhambi ya ulimwengu! 30 Huyu ndiye niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa maana alikuwapo kabla sijazaliwa.’ 31 Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini nimekuja nikibatiza kwa maji kusudi apate kufahamika kwa watu wa Israeli.”
32 Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akish uka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. 33 Mimi nisingem tambua, lakini Mungu ambaye alinituma nibatize watu kwa maji ali kuwa ameniambia kwamba, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia kutoka mbinguni na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’ 34 Mimi nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.”
Wanafunzi Wa Kwanza Wa Yesu
35 Kesho yake, Yohana alikuwapo pale pamoja na wanafunzi wake wawili. 36 Alipomwona Yesu akipita, alisema, “Tazameni! Mwana-Kondoo wa Mungu!” 37 Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yohana akisema haya, walimfuata Yesu. 38 Yesu akageuka akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?” Wakamwambia, “Rabi’ 39 Yesu akawajibu, “Njooni mkapaone!” Ilikuwa yapata saa kumi jioni. Basi wakaenda wakaona alipokuwa anaishi, wakashinda naye siku hiyo.
40 Mmojawapo wa hao wanafunzi wawili waliomfuata Yesu baada ya kusikia maneno ya Yohana, alikuwa ni Andrea, ndugu yake Simoni Petro. 41 Mara baada ya haya Andrea alikwenda kumtafuta ndugu yake akamwambia, “Tumemwona Masihi,” yaani Kristo. 42 Andrea akampeleka Simoni kwa Yesu. Yesu akamtazama, akasema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana; sasa utaitwa Kefa.” Tafsiri ya Kefa kwa Kigiriki ni Petro, maana yake ‘Mwamba’.
Yesu Anawaita Filipo Na Nathanaeli
43 Kesho yake Yesu aliamua kwenda Galilaya. Akakutana na Filipo, akamwambia, “Nifuate.” 44 Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji ambapo Andrea na Petro walikuwa wanaishi. 45 Fil ipo naye akamtafuta Nathanaeli akamwambia, “Tumekutana na Yesu wa Nazareti mwana wa Yusufu, ambaye Musa katika Torati na pia Manabii waliandika habari zake.” 46 Nathanaeli akajibu, “Je, inawezekana kitu cho chote chema kikatoka Nazareti?” Filipo akamwambia, “Njoo ukajionee mwenyewe.” 47 Yesu alipomwona Nathanaeli anakaribia, akasema, “Huyu ni Mwisraeli halisi. Hana udanganyifu wo wote.” 48 Nathanaeli akamwuliza, “Umenifaha muje? ” Yesu akamjibu, “Nilikuona wakati ulipokuwa chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.” 49 Nathanaeli akamwambia, “Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!” 50 Yesu akamwambia, “Unaamini kwa kuwa nimekuambia kwamba nili kuona chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu zaidi kuliko hilo!” 51 Ndipo akawaambia, “Ninawaambia hakika, mtaona mbingu ikifunguka, na malaika wa Mungu wakienda mbinguni na kushuka juu yangu mimi Mwana wa Adamu.”
Yesu Ahudhuria Harusi Mjini Kana
2 Siku ya tatu kulikuwa na harusi katika mji wa Kana ulioko Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo 2 na Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa pia. 3 Divai ilipowaishia, mama yake Yesu alimwambia, “Hawana divai.” 4 Yesu akamjibu, “Mama, mbona unanihusisha kwenye jambo hili? Wakati wangu bado haujafika.” 5 Mama yake akawaambia watumishi, “Lo lote atakalowaambia, fanyeni. ” 6 Basi ilikuwapo hapo mitungi sita ya kuwekea maji ya kunawa, kufuatana na desturi ya Wayahudi ya kutawadha. Kila mtungi ungeweza kujazwa kwa madebe sita au saba ya maji. 7 Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Wakaijaza mpaka juu. 8 Kisha akawaambia, “Sasa choteni maji kidogo mumpelekee mkuu wa sherehe.” Wakachota, wakampelekea. 9 Yule mkuu wa sherehe akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yame geuka kuwa divai. Hakujua divai hiyo imetoka wapi ingawa wale watumishi waliochota yale maji walifahamu. Basi akamwita bwana harusi kando 10 akamwambia, “Watu wote huwapa wageni divai nzuri kwanza kisha wakianza kutosheka huwaletea divai hafifu.
Imekuwaje wewe ukaiweka divai nzuri mpaka sasa?”
11 Hii ilikuwa ishara ya kwanza aliyofanya Yesu. Muujiza huu ulifanyika katika mji wa Kana huko Galilaya, ambako Yesu alidhi hirisha utukufu wake, na wanafunzi wake wakamwamini. 12 Baada ya haya, Yesu pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, walikwenda Kapernaumu ambapo alikaa kwa siku chache.
Yesu Alitakasa Hekalu
13 Ilipokaribia sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka, Yesu alikwenda Yerusalemu. 14 Alipoingia Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng’ombe, kondoo na njiwa, na wengine wamekaa kwenye meza zao wakifanya biashara ya kubadilishana fedha. 15 Akatengeneza mjeledi wa kamba akawafukuza wote kutoka Hekaluni pamoja na kon doo na ng’ombe; akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilish ana fedha na kuzimwaga fedha zao. 16 Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, “Watoeni hapa! Mnathubutuje kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa soko?” 17 Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa Maan diko yalisema: “Upendo wangu kwa nyumba yako utaniangamiza.”
18 Viongozi wa Wayahudi wakamwuliza, “Unaweza kutuonyesha ishara gani kuthibitisha una mamlaka ya kufanya mambo haya?”
19 Yesu akawajibu, “Livunjeni hili Hekalu, nami nitalijenga tena kwa siku tatu!”
20 Wale Wayahudi wakamjibu, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita. Wewe unasema unaweza kulijenga kwa siku tatu?”
21 Lakini yeye aliposema ‘Hekalu’ alikuwa anazungumzia mwili wake. 22 Kwa hiyo alipofufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake walikumbuka maneno haya; wakayaamini Maandiko na yale maneno ali yosema Yesu.
23 Yesu alipokuwa Yerusalemu kwenye sikukuu ya Pasaka, watu wengi waliona ishara za ajabu alizokuwa akifanya, wakamwamini. 24 Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua binadamu wote. 25 Hakuhitaji mtu ye yote amwambie lo lote kuhusu bina damu. Alijua yote yaliyokuwa mioyoni mwao.
Nikodemo Amwendea Yesu Usiku
3 Kiongozi mmoja wa Wayahudi wa kundi la Mafarisayo aitwaye Nikodemo, 2 alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunafahamu kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo, kama Mungu hayupo pamoja naye.”
3 Yesu akamjibu, “Ninakwambia hakika, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu.”
4 Nikodemo akasema, “Inawezekanaje mtu mzima azaliwe? Anaweza kuingia tena katika tumbo la mama yake na kuzaliwa mara ya pili?”
5 Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. 6 Mtu huzaliwa kimwili na wazazi wake, lakini mtu huzaliwa kiroho na Roho wa Mungu. 7 Kwa hiyo usishangae ninapokuambia kwamba huna budi kuzaliwa mara ya pili. 8 Upepo huvuma po pote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uen dako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.” 9 Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?” 10 Yesu akamwambia, “Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Waisraeli na huyaelewi mambo haya? 11 Ninakwambia kweli, sisi tunazungumza lile tunalo lijua na tunawashuhudia lile tuliloliona, lakini hamtaki kutu amini! 12 Ikiwa hamuniamini ninapowaambia mambo ya duniani, mtaniaminije nitakapowaambia habari za mbinguni? 13 Hakuna mtu ye yote ambaye amewahi kwenda juu mbinguni isipokuwa mimi Mwana wa Adamu niliyeshuka kutoka mbinguni. 14 Na kama Musa alivyomwi nua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu sina budi kuinuliwa juu 15 ili kila mtu aniaminiye awe na uzima wa milele . 16 “Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 Maana Mungu hakumtuma Mwanae kuuhukumu ulimwengu bali auokoe ulimwengu. 18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakumwamini Mwana pekee wa Mungu. 19 Na hukumu yenyewe ni kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu. 20 Kwa kuwa kila mtu atendaye maovu huchu kia nuru, wala hapendi kuja kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe. 21 Lakini kila mtu anayeishi maisha ya uaminifu huja kwenye nuru, kusudi iwe wazi kwamba matendo yake yanatokana na utii kwa Mungu.”
Yesu Na Yohana Mbatizaji
22 Baadaye, Yesu alikwenda katika jimbo la Yudea pamoja na wanafunzi wake akakaa nao kwa muda na pia akabatiza watu. 23 Yohana naye alikuwa akibatiza watu huko Ainoni karibu na Sal imu kwa sababu huko kulikuwa na maji mengi. Watu walikuwa wakim fuata huko naye akawabatiza. 24 Wakati huo Yohana alikuwa bado hajafungwa gerezani.
25 Ukazuka ubishi kati ya wanafunzi kadhaa wa Yohana na Myahudi mmoja kuhusu swala la kutawadha. 26 Basi wakamwendea Yohana wakamwambia, “Rabi, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe nga’mbo ya pili ya mto wa Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!” 27 Yohana akawa jibu, “Mtu hawezi kuwa na kitu kama hakupewa na Mungu. 28 Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema mimi si Kristo ila nimetumwa nimtangulie. 29 Bibi harusi ni wa bwana harusi. Lakini rafiki yake bwana harusi anayesimama karibu na kusikiliza, hufu rahi aisikiapo sauti ya bwana harusi. Sasa furaha yangu imekamil ika. 30 Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi niwe mdogo zaidi.”
Aliyetoka Mbinguni
31 “Yeye aliyekuja kutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote. Anayetoka duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya hapa duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya watu wote. 32 Anayashuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia lakini hakuna anayekubali maneno yake. 33 Lakini ye yote anayekubali maneno yake, anathibitisha kwamba aliyosema Mungu ni kweli. 34 Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu kwa maana Mungu amempa Roho wake pasipo kipimo. 35 Baba anampenda Mwanae na amempa mam laka juu ya vitu vyote. 36 Ye yote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele; asiyemtii Mwana hatauona uzima bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake daima.”
Yesu Na Mwanamke Msamaria
4 Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kuba tiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana. 2 Lakini kwa hakika Yesu hakubatiza, wanafunzi wake ndio waliokuwa wakibatiza watu. 3 Bwana alipopata habari hizi aliondoka Yudea akarudi Galilaya. 4 Katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria.
5 Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanae Yusufu. 6 Kisima cha Yakobo kilikuwa hapo na kwa kuwa Yesu alikuwa amechoka kutokana na safari, aliketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
7 Mama mmoja Msamaria akaja kuteka maji na Yesu akamwambia, “Naomba maji ya kunywa.” 8 Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula. 9 Yule mama akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” -Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria. 10 Yesu akamjibu, “Kama ungelifahamu Mungu anataka kukupa nini, na mimi ninayekuomba maji ya kunywa ni nani, ungeliniomba nikupe maji ya uzima.”
11 Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kuchotea maji na kisima hiki ni kirefu . Hayo maji ya uzima utay apata wapi? 12 Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”
13 Yesu akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena. 14 Lakini ye yote atakayekunywa maji nitakay ompa mimi, hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa kama chemchemi itakayobubujika maji yenye uhai na kumpa uzima wa milele.”
15 Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena na wala nisije tena hapa kuchota maji!”
16 Yesu akamjibu, “Nenda kamwite mumeo, kisha uje naye hapa.” 17 Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.” Yesu akamwam bia, “Umesema kweli kuwa huna mume. 18 Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanamume unayeishi naye sasa si mume wako!”
19 Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. 20 Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu lakini ninyi Way ahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”
21 Yesu akamjibu, “Mama, niamini; wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. 22 Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwab udu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi. 23 Lakini wakati unakuja, tena umekwisha timia, ambapo wale wanaoabudu inavyostahili watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu kwa njia hii ndio anaowataka Baba. 24 Mungu ni roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” 25 Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masihi, aitwaye Kristo, anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”
26 Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye Masihi.”
Masihi.”
27 Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kum wona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemwuliza, “Unataka nini kwake?” au “Kwa nini unazungumza naye?”
28 Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaam bia watu, 29 “Njooni mkamwone mtu aliyeniambia mambo yote nili yowahi kufanya! Je, yawezekana huyu ndiye Masihi?”
30 Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu.
31 Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Rabi, kula angalau cho chote.”
32 Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.”
33 Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?” 34 Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma, na kuikamilisha kazi yake. 35 Si mnao msemo kwamba, ‘Bado miezi minne tutavuna’? Hebu yaangalieni mashamba, jinsi mazao yalivyoiva tayari kuvunwa! 36 Mvunaji hupokea ujira wake, naye hukusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele. Kwa hiyo aliyepanda mbegu na anayevuna, wata furahi pamoja. 37 Ule msemo wa zamani kwamba , ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa. 38 Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi hiyo; ninyi mmefaidika kutokana na jasho lao!”
39 Wasamaria wengi walimwamini kutokana na ushuhuda wa yule mama alipowaambia kwamba, “Ameniambia mambo yote niliyowahi kutenda.” 40 Kwa hiyo wale Wasamaria walipokuja, walimsihi akae kwao, naye akakaa kwa siku mbili. 41 Watu wengi zaidi wakamwa mini kutokana na ujumbe wake. 42 Wakamwambia yule mama, sasa hatuamini tu kwa sababu ya yale uliyotuambia bali kwa kuwa tumem sikia sisi wenyewe, na tunajua hakika kwamba yeye ni Mwokozi wa ulimwengu.”
Yesu Amponya Mtoto Wa Afisa
43 Zile siku mbili zilipokwisha, Yesu aliondoka kwenda Gali laya. 44 Yesu mwenyewe alikwisha sema kwamba nabii haheshimiki nchini kwake. 45 Lakini alipofika, Wagalilaya walimpokea vizuri baada ya kuona mambo aliyofanya huko Yerusalemu wakati wa siku kuu, maana na wao walihudhuria.
46 Alikwenda tena mjini Kana katika Galilaya, kule alipo geuza maji kuwa divai. Na huko Kapernaumu alikuwapo afisa mmoja ambaye mtoto wake alikuwa mgonjwa. 47 Huyo afisa alipopata habari kuwa Yesu alikuwa amefika Galilaya kutoka Yudea, alikwenda akamwomba aje kumponya mwanae ambaye alikuwa mgonjwa karibu ya kufa.
48 Yesu akamwambia, “Ninyi watu hamwezi kuamini pasipo kuona ishara na miujiza?”
49 Yule afisa akajibu, “Bwana, tafadhali njoo kabla mwa nangu hajafa.” 50 Yesu akamwambia, “Nenda nyumbani, mwanao ataishi.” Yule afisa akaamini maneno ya Yesu, akaondoka kurudi nyumbani. 51 Alipokuwa bado yuko njiani, alikutana na watumishi wake wakamwambia kwamba mwanae alikuwa mzima. 52 Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.” 53 Yule baba akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Yesu alikuwa amemwambia, “Mwanao ataishi.” Kwa hiyo yeye, pamoja na jamaa yake yote wakamwamini Yesu.
54 Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Yesu alifanya aliporudi Galilaya kutoka Yudea.
Yesu Amponya Mtu Penye Bwawa La Bethzatha
5 Baada ya haya, Yesu alikwenda tena Yerusalemu kuhudhuria sikukuu mojawapo ya Wayahudi. 2 Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, pana bwawa moja ambalo kwa Kiebrania linaitwa Bethzatha ambalo lina baraza tano zenye safu za matao. 3 Wagonjwa wengi sana, vipofu, viwete, na waliopooza walingojea kwenye baraza hizo. Walikuwa wakisubiri maji yatibuliwe, [ 4 kwa maana malaika wa Bwana alikuja mara kwa mara akayatibua maji na yule aliyekuwa wa kwanza kuingia bwawani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wo wote aliokuwa nao.]
5 Mmoja wa wagonjwa waliokuwepo alikuwa ameugua kwa muda wa miaka thelathini na minane. 6 Yesu alipomwona amelala hapo, na akijua kwamba amekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu, alimwul iza, “Unataka kupona?” 7 Yule mgonjwa akajibu, “Bwana, sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Ninapoanza kwenda bwawani, mgonjwa mwingine huniwahi akaingia kabla yangu.” 8 Yesu akamwambia, “Simama, chukua mkeka wako, utembee!” 9 Mara moja yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea! Jambo hili lilitokea siku ya sabato. 10 Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni sabato. Huruhusiwi kubeba mkeka wako.”
11 Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chu kua mkeka wako utembee.”’
12 Wakamwuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako utembee?”
13 Yule mtu aliyeponywa hakufahamu ni nani aliyemponya kwa sababu palikuwa na umati mkubwa wa watu na Yesu alikuwa amepe nyezea humo akaondoka.
14 Baadaye Yesu alimkuta yule aliyemponya Hekaluni akamwam bia, “Sasa umepona. Angalia usitende dhambi tena usijepatwa na jambo baya zaidi.”
15 Yule mtu akaenda, akawaambia wale Wayahudi kuwa ni Yesu aliyemponya.
16 Kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya sabato, wal ianza kumsumbua. 17 Yesu akawaambia, “Baba yangu anafanya mema siku zote. Mimi pia sina budi kufanya mema.” 18 Maneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia wapate kumwua, kwa sababu, zaidi ya kuvunja sheria za sabato, alikuwa akijifanya sawa na Mungu kwa kujiita Mwana wa Mungu.
Mamlaka Ya Mwana
19 Yesu akawajibu, “Ninawaambia hakika, Mwana hawezi kufa nya jambo lo lote mwenyewe isipokuwa lile alilomwona Baba yake akifanya; na lo lote alifanyalo Baba, Mwana pia hulifanya. 20 Kwa kuwa Baba anampenda Mwana na anamwonyesha mambo yote afa nyayo; pia atamwonyesha hata mambo makubwa kuliko haya, ambayo yatawastaajabisha. 21 Kama vile Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo Mwana huwapa uzima wale awapendao. 22 Baba hamhukumu mtu ye yote, mamlaka ya kuhukumu amemwachia Mwana; 23 ili kila mtu amheshimu Mwana kama amheshimuvyo Baba. Ye yote anayekataa kumheshimu Mwana, anakataa kumheshimu Baba aliyemtuma. 24 Ninawaambia hakika, ye yote anayesikiliza maneno yangu na kumwamini yule aliyenituma, anao uzima wa milele na hatahukumiwa. Amevuka kutoka kwenye mauti, na kuingia katika uzima. 25 Nina waambia hakika, wakati utafika, tena umekwisha timia, ambapo wafu wataisikia sauti ya Mwana wa Mungu; na wote watakaoisikia wata kuwa hai. 26 Kama vile Baba alivyo chanzo cha uzima, hali kad halika amemwezesha Mwanae kuwa chanzo cha uzima. 27 Na amempa Mwanae mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu.
28 “Msishangae kusikia haya. Wakati unakuja ambapo wafu wataisikia sauti yake, 29 nao watatoka makaburini; wale waliot enda mema watafufuka na kuwa hai, na wale waliotenda maovu, wata fufuka na kuhukumiwa. 30 Mimi siwezi kufanya jambo lo lote kwa mamlaka yangu mwenyewe. Mimi nahukumu kufuatana na jinsi Mungu anavyoniambia. Na hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti kufa nya nipendavyo, bali nafanya mapenzi yake yeye aliyenipeleka.”
Mashahidi Wa Yesu
31 “Kama ningekuwa najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu usingekuwa na uzito. 32 Lakini yupo mwingine anishuhudiaye na ninafahamu kwamba ushuhuda wake ni wa kweli. 33 Mliwapeleka wajumbe wenu kwa Yohana, naye akashuhudia iliyo kweli. 34 Si kwamba ninategemea ushuhuda wa mwanadamu, la, bali ninalitaja hili kusudi ninyi mpate kuokolewa. 35 Yohana alikuwa taa iliy owaka na kuwaangazia, na kwa muda mlikubali kufurahia nuru yake.
36 “Lakini ninao ushuhuda mzito zaidi kuliko wa Yohana. Kazi ambayo Baba amenituma nikamilishe, naam , ishara hizi nina zofanya, zinashuhudia kuwa Baba ndiye aliyenituma. 37 Na Baba aliyenituma naye amenishuhudia. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuiona sura yake. 38 Wala ujumbe wake hamuupokei maana hamumwamini aliyemtuma.
39 “Mnasoma Maandiko kwa bidii kwa maana mnafikiri kuwa humo mtapata uzima wa milele. Maandiko hayo hayo ndio yanayonish uhudia mimi. 40 Lakini mnakataa kuja kwangu kupata uzima.
41 “Mimi sitafuti kutukuzwa na watu. 42 Lakini, ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu. 43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu na mnakataa kunipokea. Lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea. 44 Ndio maana hamwezi kuamini! Mnapenda sana kusifiana wenyewe kwa wenyewe wala ham jishughulishi kutafuta sifa kutoka kwake ambaye peke yake ndiye
Mungu!
45 “Msidhani kuwa mimi nitawashtaki kwa Baba. Anayewashtaki ni huyo Musa ambaye mnamwekea matumaini yenu. 46 Kama kweli mli kuwa mmemwamini Musa, mngaliniamini na mimi kwa maana aliandika kunihusu mimi. 47 Lakini ikiwa hamwamini aliyoandika Musa, mtaaminije ninayoyasema?”
Copyright © 1989 by Biblica