Bible in 90 Days
26 Ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa kumwamini Kristo. 27 Kwa maana nyote mliobatizwa katika Kristo, mmemvaa Kristo. 28 Hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanaume na mwanamke. Wote mmekuwa kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu. 29 Ikiwa ninyi ni wa Kristo, basi ni wa uzao wa Ibrahimu na ni warithi wa ahadi aliyopewa na
Wana Wa Mungu
4 Nataka muelewe kwamba mrithi akiwa bado ni mtoto mdogo hana tofauti na mtumwa, ingawa mali yote ni yake. 2 Kwa sababu anakuwa yuko chini ya uangalizi wa walezi na wadhamini mpaka ufike wakati uliowekwa na baba yake. 3 Hali kadhalika na sisi, tulipokuwa bado watoto wadogo, tulikuwa tunatawaliwa na kanuni za mazingira. 4 Lakini wakati ulipotimia, Mungu alimtuma Mwana we, ambaye alizaliwa na mwanamke chini ya sheria, 5 ili kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, tupate kibali cha kuwa wana wa Mungu. 6 Na kwa kuwa ninyi sasa ni wana wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae akae ndani ya mioyo yenu, akiita, “Abba! Baba.” 7 Kwa hiyo, wewe sio mtumwa tena, bali ni mwana wa Mungu, na ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, basi wewe pia ni mrithi.
Paulo Alivyowajali Wagalatia
8 Zamani, wakati hamkumjua Mungu, mlikuwa mkitumikia ‘miu ngu’ ambayo kwa asili si miungu. 9 Lakini sasa kwa kuwa mmemfa hamu Mungu, au tuseme, sasa Mungu anawafahamu ninyi, mnawezaje kurudia tena upungufu na umaskini wa nguvu za pepo muwe watumwa wake? 10 Bado mnaadhimisha siku maalumu, miezi, nyakati na miaka! 11 Nina hofu juu yenu; inaelekea kazi niliyofanya kwa ajili yenu imepotea bure.
12 Ndugu zangu, nawasihi muwe kama mimi, kwa sababu na mimi nimekuwa kama ninyi. Hamkunitendea ubaya wo wote. 13 Ninyi mnafahamu kwamba ugonjwa wangu ndio ulionipatia nafasi ya kuwa hubiria Habari Njema kwa mara ya kwanza. 14 Lakini ninyi hamku nidharau wala kunikataa ingawa udhaifu wa mwili wangu ulikuwa mzigo kwenu. Bali mlinipokea vizuri kama malaika wa Mungu, na kama Kristo Yesu. 15 Ile furaha mliyokuwa nayo iko wapi sasa? Naweza kushuhudia kwamba wakati ule mlikuwa tayari hata kung’oa macho yenu mnipe. 16 Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa sababu nawaambieni ukweli?
17 Hao watu wanaoshughulika ili muwe upande wao nia yao si nzuri. Wanataka kuwatenganisha na sisi ili muwajali wao zaidi. 18 Ni vema watu wanapowahangaikia kwa bidii kama shabaha ya kufanya hivyo ni nzuri, na kama wanafanya hivyo wakati wote, isiwe tu wakati nikiwa nanyi. 19 Watoto wangu wadogo, najisikia kwa mara nyingine kama mama mwenye uchungu wa kuzaa, nikitamani kwamba Kristo aumbike ndani yenu. 20 Natamani ningekuwa pamoja nanyi sasa, pengine ningebadilisha msemo wangu. Kwa maana nata tanishwa na hali yenu.
21 Niambieni, ninyi mnaotaka kutawaliwa na sheria, je, hamu elewi sheria inavyosema? 22 Kwa maana imeandikwa katika Maandi ko kwamba Abrahamu alikuwa na watoto wawili: mtoto mmoja alizal iwa na mwanamke mtumwa, na wa pili alizaliwa na mwanamke huru. 23 Lakini, mtoto wa mwanamke mtumwa alizaliwa kwa mapenzi ya mwili na yule wa mwanamke huru alizaliwa kutokana na ahadi ya Mungu. 24 Mambo haya yanaweza kueleweka kama mfano. Kwa maana hao mama wawili ni mfano wa maagano mawili: agano la kwanza, ni lile lililofanyika katika mlima wa Sinai, wakazaliwa watoto wa utumwa; huyo ni Hajiri. 25 Hajiri sasa anawakilisha mlima Sinai ulioko Arabuni, na ni mfano wa Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake. 26 Lakini Yerusalemu ya mbinguni ni huru, nayo ndio mama yetu. 27 Kwa maana imeandikwa: “Furahi wewe uliyetasa usiyeweza kuzaa; piga kelele, ulie kwa furaha wewe usiyepatwa na maumivu ya uzazi; kwa maana watoto wa yule ali yeachwa ni wengi kuliko watoto wa yule aliye na mume.”
28 Sasa ndugu zangu, sisi kama Isaki, tu watoto wa ahadi. 29 Lakini, kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivy omtesa yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo hata sasa. 30 Lakini Maandiko yanasemaje? “Mfukuze mwanamke mtumwa pamoja na mwanae; kwa sababu mtoto wa mtumwa hawezi kurithi pamoja na mtoto wa mwanamke huru.” 31 Kwa hiyo ndugu zangu, sisi si watoto wa mtumwa bali wa mwanamke huru. Uhuru Ndani Ya Kristo
5 Kristo alituweka sisi huru ili tuwe na uhuru. Kwa hiyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na minyororo ya utumwa. 2 Sikilizeni! Mimi Paulo nawaambieni kwamba kama mkiku bali kutahiriwa, basi Kristo hatawafaidia cho chote. 3 Tena, napenda kumshuhudia kila mmoja wenu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria zote. 4 Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria fahamuni kwamba mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu. 5 Kwa maana, kwa msaada wa Roho wa Mungu, sisi tunangojea kwa matumaini kupata haki kwa njia ya imani. 6 Kwa maana tukiwa ndani ya Kristo, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuleti faida yo yote, bali jambo la msingi ni kuwa na imani inayofanya kazi kwa upendo.
7 Mlikuwa mkienenda vizuri, sasa ni nani aliyewazuia msiitii kweli? 8 Kushawishiwa huku hakutokani na yule anayewaita. 9 Hamira kidogo sana inaweza kuchachusha donge zima. 10 Nina hakika katika Bwana kwamba mtakubaliana na msimamo wangu. Huyo anayewasumbueni atapata hukumu anayostahili hata akiwa nani. 11 Lakini ndugu zangu, kama mimi ninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwa nini bado nateswa? Ingekuwa hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingekuwa kikwazo tena. 12 Laiti hao wanaowavurugeni wangejikatakata wenyewe!
13 Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili muwe watu huru. Hata hivyo msitumie uhuru wenu kuendelea kufuata tamaa za mwili, bali tumi kianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo. 14 Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” 15 Lakini ikiwa mtaumana na kutafunana, basi jihadhar ini, msije mkaangamizana wenyewe kwa wenyewe.
Maisha Ya Kiroho
16 Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute kutimiza tamaa za mwili. 17 Kwa maana tamaa za mwili hushindana na Roho; na Roho hushindana na tamaa za mwili. Roho na mwili hupingana, na kwa sababu hiyo ninyi hamwezi kufanya yale mnayotaka. 18 Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko tena chini ya sheria.
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: uasherati, uchafu, ufisadi, 20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha waonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama haya, hawataurithi Ufalme wa Mungu. 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga mambo kama haya.
24 Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na tamaa zake. 25 Kwa kuwa tunaishi kwa kuongozwa na Roho wa Mungu, basi tufuate uongozi wake. 26 Tusiwe watu wenye maji vuno, tusichokozane na wala tusioneane wivu. Kuchukuliana Mizigo
6 Ndugu zangu, mkimwona mtu amenaswa katika dhambi fulani, basi ninyi mnaoongozwa na Roho, mrejesheni mtu huyo kwa upole. Lakini mjihadhari, ili na ninyi msije mkajaribiwa. 2 Chukulianeni mizigo yenu; na kwa njia hiyo mtaweza kutimiza sheria ya Kristo. 3 Mtu akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe siyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe. 4 Lakini, kila mtu apime mwenendo wake, ndipo anaweza kuwa na sababu ya kujisifu bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine. 5 Kwa maana, kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe. 6 Basi, mwanafunzi na amshirikishe mwalimu wake vitu vyote vilivyo vyema.
7 Msidanganyike, Mungu hadanganywi. Kwa maana kila mtu ata vuna kile alichopanda. 8 Mtu apandaye katika tamaa za mwili, ata vuna kutoka katika mwili uharibifu; lakini yeye apandaye katika Roho, atavuna kutoka katika Roho uzima wa milele. 9 Basi, tusi choke kutenda mema, kwa sababu kama hatukuchoka tutavuna kwa wakati wake. 10 Kwa hiyo basi, kadiri tunavyopata nafasi, tuwa tendee mema watu wote, na hasa wale tunaoshiriki imani moja.
Maonyo Ya Mwisho Na Salamu
11 Tazameni jinsi maandishi ya mkono wangu mwenyewe yalivyo makubwa. 12 Ni wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaowalazimisheni mtahiriwe; na wanafanya hivyo ili wao wenyewe wasije kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Kristo. 13 Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawashiki sheria; lakini wanataka na ninyi mtahiriwe ili wapate kujivunia hiyo alama katika miili yenu. 14 Lakini mimi kamwe sitajivunia kitu cho chote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo; kwa maana kwa njia ya msalaba, ulimwengu umesulubiwa kwangu, na mimi nimesulubiwa kwa ulimwengu. 15 Kwa maana, kutahiriwa au kutota hiriwa si kitu kwangu; kitu cha maana ni maisha ya watu kubadili ika kuwa mapya. 16 Amani na rehema ya Mungu ikae na wote wanao fuata kanuni hii, na kwa Israeli ya kweli ya Mungu.
17 Basi, tangu sasa mtu ye yote asije akanisumbua, kwa sababu ninazo alama za Yesu mwilini mwangu.
1 Kutoka kwa Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu. Kwa watu wa Mungu walio waaminifu kwa Kristo Yesu. 2 Nawa takieni neema ya Mungu na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 3 Asifiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametu bariki sisi kwa kila baraka za kiroho zitokazo mbinguni tukiwa ndani ya Kristo. 4 Mungu alituchagua sisi tuwe ndani ya Kristo hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na lawama mbele zake. 5 Kwa upendo wake, alipanga kabla ya mambo yote, kutufanya sisi kuwa watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo kwa mapenzi yake mwenyewe; 6 na hivyo apewe sifa kwa ajili ya neema yake tukufu ambayo tumepewa bure katika Mpendwa wake. 7 Kutoka kwake, tunapata ukombozi kwa ajili ya damu yake, yaani, kusamehewa dhambi zetu; kulingana na wingi wa neema yake 8 ambayo ametumiminia kwa wingi. 9 Kwa maana ametufahamisha kwa hekima yote na ufahamu, siri ya mapenzi yake, kulingana na mpango aliokusudia kuukamilisha kwa njia ya Kristo. 10 Mpango huo ambao ungetekelezwa wakati ukitimia, ni kwamba Mungu ataviunganisha vitu vyote po pote vilipo, mbinguni na duniani, viwe kwake chini ya Kristo. 11 Tukiwa ndani ya Kristo, tulichaguliwa kama alivy opanga Mungu kwa makusudio yake yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na mapenzi yake. 12 Kwa njia hiyo, sisi ambao tulikuwa wa kwanza kumtegemea Kristo, tupate kuishi maisha yatakayoleta sifa kwa utukufu wake. 13 Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Nanyi mmemwa mini, mkawekewa muhuri na Roho Mtakatifu ambaye mliahidiwa, 14 yeye ndiye dhamana ya urithi wetu mpaka hapo tutakapoupokea, kwa sifa ya utukufu wake. Shukrani Na Maombi
15 Hii ndio sababu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana wetu Yesu, na juu ya upendo mlio nao kwa watu wa Mungu, 16 sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, na kuwakumbuka katika sala zangu. 17 Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni roho ya hekima na ya mafunuo mpate kumfahamu zaidi. 18 Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yaangaziwe ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, na mtambue utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watu wa Mungu; 19 na muu fahamu uweza wake usiopimika ambao ametupa sisi tunaoamini. Uweza huo ni sawa na ile nguvu kuu 20 ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamweka akae mkono wake wa kulia katika enzi yake mbinguni. 21 Hapo alipo ni juu sana, kupita tawala na mamlaka zote na nguvu zote na milki, na kupita cheo cho chote kinachoweza kutolewa, si tu katika nyakati hizi, bali pia katika nyakati zijazo. 22 Na Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya mamlaka yake na akamteuwa awe mkuu wa vitu vyote kwa ajili ya kanisa, 23 ambalo ni mwili wake, nalo limejawa na yeye ambaye hujaza kila kitu kwa kila njia. Tumefanywa Kuwa Hai Ndani Ya Kristo
2 Nanyi aliwafanya muwe hai, mlipokuwa mmekufa kiroho kwa ajili ya makosa na dhambi zenu. 2 Hapo zamani mliishi maisha ya jinsi hiyo, mkimtii mfalme wa nguvu za anga, ambaye ndiye ile roho inayowatawala wote wanaomwasi Mungu. 3 Sisi sote pia tuliishi miongoni mwao hapo zamani, tukiridhisha na kutawaliwa na tamaa mbaya za mwili na mawazo. Kwa hiyo sisi pia tulikuwa kwa asili tunastahili ghadhabu ya Mungu kama binadamu wengine wote. 4 Lakini Mungu, ambaye ana huruma nyingi, kutokana na upendo wake mkuu ambao alitupenda nao, 5 japokuwa tulikuwa bado tumekufa kiroho kwa sababu ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu. Mmeokolewa kwa neema. 6 Mungu alitufufua pamoja na Kristo, akatufanya tukae pamoja naye katika makao ya mbinguni tukiwa ndani yake Kristo; 7 ili katika vizazi vijavyo aonyeshe wingi wa neema yake isiyo na mfano, ambayo imedhihirishwa kwa wema wake kwetu sisi tunaoishi ndani ya Kristo Yesu. 8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na si kwa sababu ya matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. 9 Na kwa sababu hamkuifanyia kazi, mtu ye yote asije akajisifu juu ya wokovu wake. 10 Kwa maana sisi ni matokeo ya kazi ya Mungu tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tuwe na matendo mema ambayo Mungu alikwisha andaa, tuishi katika hayo. 11 Kwa hiyo kumbukeni kwamba ninyi ambao kwa asili ni watu wa mataifa mengine, mnaoitwa ‘wasiotahiriwa’ na wale ‘waliotahi riwa’ kwa kanuni za binadamu; 12 kumbukeni kwamba wakati ule ninyi mlikuwa mmetengwa na Kristo, mkiwa mmefarakana na jumuia ya Israeli na mkiwa wageni kuhusu yale maagano ya ahadi. Mlikuwa hamna matumaini wala Mungu duniani. 13 Lakini kwa kuwa mmeungana na Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali zamani, sasa mmeletwa karibu kwa njia ya damu ya Kristo. 14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu; yeye aliyetufanya tuwe jamii moja, akavunjavunja ule ukuta wa uadui uliotutenga 15 kwa kuifuta ile sheria na amri zake na kan uni zake alipoutoa mwili wake. Alifanya hivyo ili aumbe taifa jipya kutokana na jamii mbili: Wayahudi na watu wa mataifa, na hivyo alete amani. 16 Kwa kutoa mwili wake pale msalabani, ali patanisha jamii zote mbili na Mungu; na kwa njia hiyo akaua ule uadui uliokuwepo kati yao. 17 Alikuja akahubiri amani kwenu ninyi watu wa mataifa ambao mlikuwa mbali na Mungu, na pia kwa wale waliokuwa karibu na Mungu. 18 Kwa maana, kwa kupitia kwake, sisi sote, Wayahudi na watu wa mataifa, tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja. 19 Kwa hiyo, ninyi sasa siyo wageni tena wala wapita njia, bali mmekuwa raia halisi pamoja na watu wa Mungu na familia ya Mungu. 20 Ninyi mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni. 21 Ndani yake yeye, jengo lote limeunganishwa pamoja na kusimam ishwa kuwa Hekalu takatifu la Mungu. 22 Katika yeye ninyi pia mnajengwa pamoja ili mpate kuwa makao ambamo Mungu anaishi kwa njia ya Roho wake. Paulo, Mhudumu Kwa Watu Wa Mataifa
3 Kwa sababu hii, mimi Paulo, nimekuwa mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi watu wa mataifa. 2 Ninaamini kwamba mmek wisha sikia kuwa Mungu amenipa neema yake niwe mhudumu kwa ajili yenu; 3 na kwamba Mungu alinifahamisha siri hii kwa njia ya mafu nuo, kama nilivyokwisha andika kwa kifupi. 4 Kwa hiyo mtakaposoma barua hii mtaweza kutambua ufahamu niliopewa kuhusu siri ya Kris to. 5 Siri hii haikufahamika kwa watu wa vizazi vilivyopita kama ilivyodhihirishwa sasa na Roho kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu. 6 Siri hii ni kwamba, kwa njia ya Injili, watu wa mataifa ni warithi pamoja na Waisraeli; na wote pamoja ni viungo vya mwili mmoja, na ni washiriki kwa pamoja wa ile ahadi aliyotoa Mungu katika Kristo Yesu. 7 Niliteuliwa kuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa uwezo wake uliokuwa ukifanya kazi ndani yangu. 8 Ingawa mimi ni mdogo kuliko hata aliye mdogo kabisa kati ya watu wote wa Mungu, nilipewa neema hii, niwahubirie watu wa mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo. 9 Na nieleze wazi wazi ili watu wote waone jinsi siri hii itakavyotekelezwa. Siri hii ilikuwa imefichwa tangu awali kwa Mungu aliyeumba vitu vyote. 10 Yeye alikusudia kwamba sasa, kwa njia ya kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kufa hamika kwa mamlaka na nguvu zote katika makao ya mbinguni. 11 Mpango huu ulikuwa sawasawa na mapenzi yake yaliyotimi zwa katika Kristo Yesu Bwana wetu, 12 ambaye tukiwa ndani yake, tuna ujasiri na uhakika wa kumkaribia Mungu kwa njia ya imani katika Kristo. 13 Kwa hiyo, nawasihi msikate tamaa kutokana na mateso ninayopata kwa ajili yenu; mateso haya ni utukufu wenu. Sala Ya Paulo Kwa Waefeso
14 Kwa sababu hii napiga magoti mbele ya Mungu Baba, 15 aliye baba wa familia ya waamini wote, mbinguni na duniani. 16 Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyoni mwenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake. 17 Na naomba kwamba, kwa imani, Kristo aendelee kuishi ndani ya mioyo yenu, ili mkiwa mmesimama imara na kujengwa katika upendo, 18 mpate uwezo wa kuelewa, pamoja na watu wote wa Mungu, upana na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo; 19 na mpate kufa hamu upendo huu, ingawa unapita upeo wa maarifa, na hivyo mpate kujazwa kabisa na ukamilifu wa Mungu mwenyewe. 20 Utukufu ni wake yeye, ambaye ana uwezo wa kutenda zaidi ya yale tunayoyaomba na kuyawazia, kwa kadiri ya nguvu yake inayofanya kazi ndani yetu. 21 Utukufu ni wake katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amina.
4 Basi, mimi niliye mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mu ishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa. 2 Muwe wanyenyekevu, wapole, wenye subira, mkivumiliana ninyi kwa ninyi katika upend o. 3 Muwe wepesi wa kutaka kudumisha umoja wa Roho kwa sababu ya amani inayowafunga pamoja. 4 Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, k ama mlivyoitwa mpokee tumaini moja. 5 Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja; 6 na Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wot e, aliye juu ya wote, anayefanya kazi katika yote na aliye ndani ya yote. 7 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo alichogawiwa na Kristo. 8 Kwa hiyo Maandiko yanasema: “Alipopaa juu, aliongoza mateka wengi, na akawapa watu zawadi.” 9 Maandiko yanaposema, “Alipaa juu’ 10 Yeye aliyeshuka ndiye aliyepaa juu sana, kupita mbingu zote, ili apate kujaza vitu vyote. 11 Yeye ndiye aliyewapa watu vipawa, wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji na walimu; 12 wapate kuwatayarisha watu wa Mungu kwa kazi za huduma, kwa ajili ya kujenga kanisa, ambalo ni mwili wa Kristo. 13 Kazi hiyo itaende lea mpaka sote tuufikie umoja katika imani na katika kumjua Mwana wa Mungu; tupate kuwa watu waliokomaa kiroho kwa kufikia kiwango cha ukamilifu wote ulio ndani ya Kristo. 14 Hapo ndipo tutaacha kuwa tena kama watoto wadogo, wanaorushwarushwa huku na huko na kupeperushwa na kila upepo wa mafundisho na hila za watu wadan ganyifu. 15 Badala yake, tukiambiana ukweli kwa upendo, tutakua kwa kila hali, tufanane na Kristo ambaye ndiye kichwa. 16 Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeunganishwa na kushikamanishwa pamoja kwa viungo vyake, hukua na kujengeka katika up endo, kila sehemu ikifanya kazi yake. Maisha Mapya Ndani Ya Kristo
17 Kwa hiyo nawaambia na kusisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu wa mataifa wasiomjua Mungu, ambao wanaon gozwa na mawazo yao yasiyofaa. 18 Watu hao akili zao zimetiwa giza wasiweze kuelewa; nao wametengwa mbali na uhai wa Mungu kwa sababu ya ujinga walionao na ugumu wa mioyo yao. 19 Kwa kuwa hawajali kuhusu mema na mabaya, wamekuwa sugu na kutawaliwa na uasherati, wakiwa na tamaa ya kutenda kila aina ya uchafu. 20 Lakini ninyi hamkujifunza hivyo kutoka kwa Kristo, 21 kama kweli mlisikia habari zake na kufundishwa kumhusu, kufuatana na kweli itokayo kwa Yesu. 22 Vueni maisha yenu ya zamani muweke kando hali yenu ya asili ambayo huharibiwa na tamaa potovu. 23 Nia zenu zifanywe upya 24 na mvae utu upya ulioumbwa kwa mfano wa Mungu katika haki na utakatifu. 25 Kwa hiyo, kila mmoja wenu aache kusema uongo, na amwambie ndugu yake ukweli, kwa maana sisi sote ni viungo vya mwili mmoja. 26 Mkikasirika, msitende dhambi; msikubali kukaa na hasira kutwa nzima 27 na kumpa she tani nafasi. 28 Mwizi asiibe tena, bali afanye kazi halali kwa mikono yake ili aweze kuwa na kitu cha kuwapa wenye kuhitaji msaada. 29 Msiruhusu maneno machafu yatoke vinywani mwenu, bali mazungumzo yenu yawe ya msaada katika kuwajenga wengine kufuatana na mahitaji yao, ili wale wanaowasikiliza wapate kufaidika. 30 Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye ni mhuri wenu wa uthibitisho kwa siku ya ukombozi. 31 Ondoeni kabisa chuki yote, ghadhabu, hasira, ugomvi na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. 32 Muwe wema na wenye mioyo ya upendo kati yenu, na kusameheana kama Mungu alivyowasamehe kwa ajili ya Kristo. Watoto Wa Nuru
5 Kwa hiyo mfuateni Mungu kama watoto wapendwa. 2 Muishi maisha ya upendo kama Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu. 3 Lakini uasherati, uchafu wa aina zote na tamaa, wala yasitajwe miongoni mwenu, kwa maana mambo haya hayawastahili watakatifu wa Mungu. 4 Kusiwepo na mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuuzi au mzaha; mazungumzo ya namna hii hayafai. Badala yake mshukuruni Mungu. 5 Mjue hakika kwamba hakuna mwasherati wala mtu mwenye mawazo machafu, wala mwenye tamaa, yaani mwabudu sanamu, ambaye ataurithi Ufalme wa Kristo na wa Mungu. 6 Msikubali kudan ganywa na mtu ye yote kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juu ya watu wote wasiomtii. 7 Kwa hiyo, msishirikiane nao. 8 Zamani ninyi pia mlikuwa gizani, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana; basi muishi kama watoto wa nuru. 9 Kwa maana tunda la nuru hupatikana katika kila lililo jema, lililo la haki na la kweli. 10 Jifunzeni mambo yanayom pendeza Bwana. 11 Msishiriki matendo ya giza yasiyofa a, bali yafichueni. 12 Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo wanayofanya kwa siri. 13 Lakini ikiwa jambo lo lote linawekwa katika nuru, huonekana, kwa maana ni nuru inayofanya vitu vionekane. 14 Ndio sababu husemwa, “Amka wewe uliyelala, ufufuke kutoka kwa wafu, na Kristo atakuangazia.” 15 Kwa hiyo muwe waangalifu jinsi mnavyoishi; msiishi kama watu wasio na hekima, bali kama watu wenye hekima, 16 mkitumia vizuri muda mlio nao, kwa maana hizi ni nyakati za uovu. 17 Kwa hiyo msiwe wajinga, bali muelewe yaliyo mapenzi ya Mungu. 18 Pia msilewe divai, kwa sababu huo ni upotovu, bali mjazwe Roho. 19 Zungumzeni ninyi kwa ninyi kwa zaburi na nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia Mungu mioyoni mwenu kwa sauti tamu. 20 Wakati wote na kwa kila kitu mshukuruni Mungu Baba katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. 21 Kila mmoja wenu ajinyenyekeze kwa mwenzake kwa sababu ya upendo mlio nao kwa Kristo. 22 Wake, watiini waume zenu kama mnavyomtii Bwana. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mke kama vile Kristo alivyo kichwa cha kanisa, ambalo ni mwili wake, naye mwe nyewe ni Mwokozi wa kanisa. 24 Basi, kama vile Kanisa linavyom tii Kristo, vivyo hivyo na wake pia wanapaswa kuwatii waume zao kwa kila jambo. 25 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda kanisa akajitoa nafsi yake kwa ajili yake ili 26 alitakase. Alifanya hivyo kwa kuliosha kwa maji na kwa neno lake 27 ili ajipatie kanisa linalong’aa, lisilo na doa wala kunjamano wala kitu kingine cho chote kama hicho; liwe takatifu na bila kasoro. 28 Vivyo hivyo waume wawapende wake zao kama miili yao. Anayempenda mkewe anajipenda mwenyewe. 29 Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza kanisa lake. 30 Sisi tu viungo vya mwili wake. 31 “Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataungana na mkewe, na hawa wawili wata kuwa mwili mmoja.” 32 Hili ni fumbo gumu kueleweka, nami nasema kuwa ni kielelezo kuhusu Kristo na kanisa. 33 Hata hivyo kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake; na mke naye ahakikishe anamheshimu mumewe. Watoto Na Wazazi
6 Watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana kufanya hivyo ni vizuri. 2 “Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, 3 “upate baraka na uishi siku nyingi duniani.” 4 Akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana. Watumwa Na Mabwana
5 Watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani, kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnamtii Kristo. 6 Watiini, sio tu wakati wakiwaona ili mpate sifa, bali mtumike kama watumishi wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. 7 Toeni huduma yenu kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na sio watu. 8 Mkumbuke kuwa Bwana atampa kila mmoja tuzo kutegemeana na wema aliotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru. 9 Nanyi mabwana watendeeni watumwa wenu kwa jinsi hiyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua ya kwamba yeye aliye Bwana wenu na wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo.
10 Hatimaye, muwe imara katika Bwana na katika nguvu zake kuu. 11 Vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama na kupin gana na hila zote za shetani. 12 Kwa maana hatupambani na bina damu, bali tunapambana na tawala na mamlaka na nguvu za ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama imara siku ya uovu itakapokuja; na mkishafanya yote, mtakuwa bado mme simama. 14 Kwa hiyo simameni imara mkisha jifunga na kweli kama mkanda kiunoni na haki kama kinga ya kifuani; 15 na kuvaa Injili ya amani kama viatu miguuni, ili muweze kusimama barabara. 16 Zaidi ya haya yote, jivikeni imani kama ngao ambayo itawawe zesha kuzuia mishale yenye miale ya moto kutoka kwa yule mwovu. 17 Vaeni wokovu kama kofia ya vita vichwani na chukueni upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu. 18 Ombeni wakati wote katika Roho, katika sala zote na maombi. Kwa hiyo muwe macho na siku zote endeleeni kuwaombea watu wote wa Mungu. 19 Niombeeni mimi pia, ili kila ninapozungumza, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili pasipo woga. 20 Mimi ni balozi kifun goni kwa ajili ya Injili hii. Kwa hiyo niombeeni niihubiri Injili kwa ujasiri kama inipasavyo. 21 Ndugu mpendwa Tikiko, ambaye ni mtumishi mwaminifu wa Bwana, atawaelezeni kila kitu ili mjue habari zangu na mfahamu ninachofanya. 22 Ninamtuma kwenu kwa kusudi hili, mpate habari zetu naye awafariji. 23 Nawatakia ndugu wote amani na upendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo.
1 Kutoka kwa Paulo na Timotheo, watumwa wa Yesu Kristo. Kwa watakatifu walioko Filipi pamoja na maaskofu na wasaidizi wote wa kanisa. 2 Tunawatakieni neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Shukrani Na Maombi.
3 Ninamshukuru Mungu wangu kila ninapowakumbuka 4 katika sala zangu zote, nikiomba kwa furaha 5 na shukrani kwa ajili ya ushi rikiano uliopo kati yetu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo. 6 Nina hakika kwamba, yeye aliyeianza kazi yake njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha siku ile ataka porudi Yesu Kristo.
7 Ninajisikia hivi kwa sababu nawathamini sana moyoni mwangu. Kwa maana tumeshiriki pamoja neema ya Mungu wakati nikiwa kifun goni na wakati nikiitetea na kuithibitisha Injili. 8 Mungu ni shahidi wangu kwamba natamani mno kuwa pamoja nanyi na kwamba upendo nilio nao kwenu ni upendo wa Kristo Yesu. 9 Na sala yangu kwa ajili yenu ni kwamba upendo wenu uzidi kuongezeka siku hadi siku pamoja na maarifa na busara 10 ili mpate kutambua mambo yaliyo mema. Na pia mpate kuwa watu safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo. 11 Maisha yenu yawe na matunda ya haki yatokayo kwa Yesu Kristo, ili Mungu apewe utukufu na sifa. 12 Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba haya mambo yaliyonipata yamesaidia sana kueneza Injili ya Kristo. 13 Watu wote hapa pamoja na maaskari wa ikulu wanajua wazi kuwa mimi niko kifungoni kwa sababu ya kumtumikia Kristo. 14 Kwa sababu ya kifungo changu, ndugu wengi katika Bwana wametiwa moyo kuhubiri neno la Mungu pasipo hofu. 15 Ni kweli kwamba wapo ndugu wengine wanaom hubiri Kristo kutokana na wivu na kwa kutaka kushindana; lakini wengine wanamhubiri Kristo kwa nia njema. 16 Hawa wanahubiri kwa moyo wa upendo, wakifahamu kwamba Mungu ameniweka hapa kifungoni ili niitetee Injili. 17 Hao wengine wanamtangaza Kristo kwa tamaa ya kupata sifa wala si kwa moyo wa upendo, wakifikiri kwamba kwa kufanya hivyo wataniongezea mateso yangu kifungoni. 18 Lakini kwangu mimi hiyo si kitu. Lililo la muhimu ni kwamba kwa kila njia Kristo anahubiriwa, ikiwa kwa nia mbaya au kwa nia njema. Kwa sababu hiyo, mimi nashangilia. Pia nitaendelea kushan gilia, 19 kwa sababu najua kwamba kwa ajili ya sala zenu na kwa msaada wa Roho wa Yesu Kristo, jambo lililonipata litageuka kuwa njia ya kufunguliwa kwangu. 20 Shauku yangu na tumaini langu ni kwamba sitaaibika kwa njia yo yote, bali nitakuwa na ujasiri, ili kama ilivyo sasa, Kristo aendelee kutukuzwa kutokana na maisha yangu, kama ni kuishi au hata kama ni kufa. 21 Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida. 22 Kama nitaendelea kuishi katika mwili, hii itaniwezesha kufanya kazi yenye matunda. Lakini sijui nichague lipi! 23 Yote mawili yananivutia: nata mani niyaache maisha haya ili nikakae pamoja na Kristo, jambo ambalo naona ni bora zaidi. 24 Lakini kwa sababu yenu naona kuwa ni muhimu zaidi nikiendelea kuishi. 25 Nina hakika kwamba, kwa sababu hii nitabaki na kuendelea kuishi pamoja nanyi nyote, ili mpate kukua na kuwa na furaha katika imani. 26 Na hivyo, kwa ajili yangu, muwe na sababu ya kuona fahari ndani ya Kristo Yesu kwa kuja kwangu kwenu.
Mapambano Kwa Ajili Ya Imani
27 Lakini hata ikitokea nini, hakikisheni kuwa mwenendo wenu unalingana na Injili ya Kristo. Ili kama nikija kuwaona au hata nisipojaliwa kufika, nipate habari kuwa mnasimama imara katika roho ya umoja, mkiwa na nia moja huku mkipambana kwa pamoja kwa ajili ya imani ya Injili, 28 bila kuwaogopa wale wanaowapinga. Hii ni ishara dhahiri ya kuangamia kwao, lakini kwenu ninyi, hii ni ishara ya wokovu wenu kutoka kwa Mungu. 29 Kwa maana mmepewa heshima kwa ajili ya Kristo, sio tu kumwamini, bali pia kuteswa kwa ajili yake. 30 Sasa mnashiriki mapambano yale yale mliyoona nikiwa nayo na ambayo mnasikia kwamba bado naendelea nayo.
Unyenyekevu Na Ukuu Wa Kristo
2 Ikiwa mmepata faraja kwa kuwa mmeunganishwa na Kristo, kama mmevutwa na upendo wake na kushiriki Roho wake, kama mnaoneana huruma na kusaidiana; 2 basi kamilisheni furaha yangu kwa kuwa na nia moja, upendo mmoja na kuwa wamoja katika roho na shabaha. 3 Msifanye jambo lo lote kwa ajili ya ubinafsi au kwa kujiona, bali kuweni wanyenyekevu, mkiwahesabu wengine kuwa bora kuliko ninyi. 4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu ajishughulishe pia kwa faida ya wengine. 5 Muwe na nia kama ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu; 6 yeye kwa asili alikuwa sawa na Mungu, lakini hakuona kwamba kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kush ikilia sana. 7 Bali alikubali kuacha vyote, akachukua hali ya mtumishi, akazaliwa na umbo la wanadamu. 8 Alipochukua umbo la mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii mpaka kufa, tena kifo cha msalaba. 9 Kwa sababu hiyo, Mungu alimwinua juu kabisa, akampa jina ambalo ni kuu kuliko majina yote; 10 ili kwa jina la Yesu, kila goti lipigwe, mbinguni na duniani na kuzimu; 11 na kila ulimi ukiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu
Ng’aeni Kama Nyota
12 Basi rafiki zangu wapendwa, kama ambavyo mmekuwa mkitii nilipokuwa nanyi, nawasihi mwendelee kunitii vivyo hivyo, na hata zaidi sasa kwa kuwa sipo pamoja nanyi. Endeleeni kufanya bidii kwa ajili ya wokovu wenu huku mkitetemeka na kuogopa. 13 Kwa maana ni Mungu ambaye anatenda kazi ndani yenu, akiwapa nia ya kutimiza mapenzi yake na kuwawezesha kutenda yale yanayompendeza 14 Fanyeni mambo yote bila manung’uniko au mabishano 15 ili msiwe na lawama au kosa bali muwe wana wa Mungu wasio na kasoro katika ulimwengu uliopotoka, mking’aa kama nyota angani, 16 na kusisitiza neno la uzima. Mkifanya hivyo siku ya Kristo nitajisi fia kwamba sikupiga mbio au kufanya kazi bure. 17 Hata kama damu yangu itamwagwa kama sadaka juu ya dhabihu na huduma inayotokana na imani yenu, mimi ninafurahi na kushangilia pamoja nanyi nyote. 18 Vivyo hivyo, nanyi pia mnapaswa kufurahi na kushangilia pamoja nami.
Safari Ya Timotheo Na Epafrodita
19 Nina matumaini katika Bwana Yesu ya kumtuma Timotheo hivi karibuni aje kwenu, ili nipate habari za kunitia moyo kutoka kwenu. 20 Sina mtu mwingine hapa kama yeye, anayewatakieni mema kwa moyo wote. 21 Wengine wanajishughulisha zaidi na mambo yao wenyewe na hawajali lo lote kuhusu kazi ya Yesu Kristo. 22 Lakini ninyi wenyewe mnajua jinsi Timotheo alivyojithibit isha, kwa maana amefanya kazi ya Injili pamoja nami kama vile mtoto na baba yake. 23 Kwa hiyo, natumaini kumtuma Timotheo kwenu mara tu nipatapo habari kuhusu mambo yangu yatakavyokuwa. 24 Nami naamini katika Bwana kwamba mimi mwenyewe nitakuja kwenu hivi karibuni.
25 Nimeona vema kumrudisha ndugu yangu Epafrodita kwenu. Yeye ni mtumishi na askari mwenzangu, ambaye pia ni mjumbe wenu mliyemtuma anihudumie katika mahitaji yangu. 26 Yeye ana hamu kuwaoneni ninyi nyote, na amesikitishwa kwa sababu mlipata habari kwamba alikuwa mgonjwa. 27 Hakika alikuwa mgonjwa, tena karibu ya kufa. Lakini Mungu alimhurumia, na si yeye tu, bali hata na mimi alinihurumia, nisipatwe na huzuni juu ya huzuni . 28 Kwa hiyo napenda kumtuma kwenu ili mtakapomwona kwa mara nyingine, mpate kufurahi, na mimi nipunguziwe wasiwasi wangu. 29 Kwa hiyo mpokeeni katika Bwana kwa furaha kubwa; na wapeni heshima watu kama hawa. 30 Kwa maana alikaribia kufa kwa ajili ya kazi ya Kristo; alihatarisha maisha yake ili aweze kunipa msaada ambao ninyi msingeweza kunipa.
Njia Ya Kweli Ya Wokovu
3 Hatimaye ndugu zangu, furahini katika Bwana. Mimi sichoki kuwaandikieni mambo yale yale niliyokwisha waandikia kwa maana najua kwamba yatakuwa ni kinga kwenu. 2 Jihadharini na watenda maovu, hao mbwa, na wale wanaokaza mafundisho ya kutahiriwa. 3 Sisi tumepokea tohara ya kweli, kwa maana tunamwabudu Mungu katika Roho. Sisi tunaona fahari kwa ajili ya maisha yetu ndani ya Kristo Yesu. Hatuweki matumaini yetu katika mambo ya mwili, 4 ijapokuwa mimi mwenyewe ninazo sababu za kuweka matumaini katika mambo hayo. Kama mtu mwingine ye yote anadhani kuwa anazo sababu za kuweka matumaini yake katika mambo ya mwili, basi mimi ninazo sababu zaidi. 5 Nilitahiriwa siku ya nane, mimi ni Mwis raeli wa kabila la Benjamini; Mwebrania halisi. Kuhusu mambo ya kushika sheria, mimi nilikuwa Mfarisayo; 6 na kwa upande wa juhudi, mimi nilikuwa na bidii katika kutesa kanisa; na kuhusu haki ipatikanayo kwa kutii sheria, mimi nilikuwa sina hatia.
7 Lakini mambo hayo niliyoyaona mwanzo kuwa ni faida kwangu, sasa nayaona kuwa ni hasara kwa ajili ya Kristo. 8 Zaidi ya hayo, nahesabu mambo yote kuwa hasara tupu yakilinganishwa na faida kubwa ninayopata kwa kumjua Kristo Yesu aliye Bwana wangu. Kwa ajili yake nilikubali kupoteza kila kitu na kuona mambo hayo yote kuwa ni takataka ili nipate faida ya kuwa na Kristo; 9 na nikiwa kwake nisionekane kama mtu mwenye haki yake mwenyewe, inayotokana na kushika sheria, bali niwe na ile haki inayotokana na kumwamini Kristo, ambaye yeye ni haki itokayo kwa Mungu inayopatikana kwa imani. 10 Nataka nimjue Kristo na nguvu ya ufufuo wake na nishi riki mateso yake, niwe kama yeye katika kifo chake; 11 na hivyo, kama ikiwezekana, niufikie ufufuo kutoka kwa wafu.
12 Sisemi kwamba nimekwisha kupokea haya yote, au kwamba nimekwisha kuwa mkamilifu, la hasha; bali nazidi kukaza mwendo ili nipate kile ambacho, kwa ajili yake, Kristo amenifanya niwe wake. 13 Ndugu zangu, bado sijihesabu kuwa nimekwisha pata ile zawadi. Lakini jambo moja ninalofanya ni kusahau mambo yote yali yopita, na kukaza mwendo kufikia yaliyo mbele yangu. 14 Nakaza na nifikie ushindi, ili nipate zawadi ambayo Mungu ameniitia mbinguni, nikiwa ndani ya Kristo Yesu.
15 Sisi tuliokomaa kiroho tuwe na msimamo kama huu. Lakini kama kuna mawazo tofauti kuhusu jambo lo lote, Mungu atawafunu lia. 16 Ila tushike sana yale tuliyokwisha kupokea.
17 Ndugu zangu, nawasihi mfuate mfano wangu, na muwatazame wale wanaofuata mfano tuliowapa. 18 Kwa maana, kama nilivyok wisha waambia kabla, na sasa nasema tena kwa machozi, wako watu wengi miongoni mwenu ambao maisha yao yanaonyesha kuwa wao ni adui wa msalaba wa Kristo. 19 Mwisho wa watu hao ni kuangamia, na Mungu wao ni tumbo; kwa sababu wao huyaonea fahari mambo ya aibu na mawazo yao yametawaliwa na mambo ya dunia. 20 Lakini uraia wetu uko mbinguni. Nasi tunangoja kwa hamu Mwokozi kutoka huko, yaani Bwana wetu Yesu Kristo, 21 ambaye, kwa uwezo unaomwezesha kutawala kila kitu, atabadilisha miili yetu midhaifu ili iwe na utukufu kama alionao yeye.
Muwe Na Umoja, Furaha Na Amani
4 Kwa hiyo ndugu zangu wapendwa, ninaotamani mno kuwaona; ninyi ambao ni furaha yangu na taji yangu, hivi ndivyo mnavyop aswa kusimama imara katika Bwana. 2 Nawasihi Euodia na Sintike wapatane katika Bwana. 3 Na wewe ndugu yangu uliye mwaminifu katika Bwana, nakuomba uwasaidie hawa akina mama, kwa maana wame fanya kazi ya kueneza Injili kwa bidii wakiwa nami pamoja na Kle menti na watumishi wenzangu wengine, ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.
4 Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini! 5 Upole wenu ufahamike kwa watu wote. Bwana anakaribia kuja. 6 Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushu kuru 7 Na amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote, italinda mioyo yenu na nia zenu kwa Kristo Yesu.
8 Hatimaye ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo na sifa, yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote ya kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo uzuri wo wote, pakiwepo na cho chote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo. 9 Mambo yote mliyojifunza au kupokea au kusikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatekelezeni. Na Mungu wa amani ata kuwa pamoja nanyi. 10 Nina furaha kubwa katika Bwana kwa maana hatimaye mmeanza tena kunikumbuka. Kusema kweli mmekuwa mkinikum buka lakini mlikuwa hamjapata nafasi ya kuonyesha upendo wenu. 11 Sisemi hivyo kwa sababu nahitaji kitu, la. Kwa maana nimeji funza kuridhika katika hali yo yote niliyo nayo. 12 Nimepata kupungukiwa, pia nimepata kuwa na wingi wa vitu. Nimejifunza siri ya kuridhika katika kila hali, wakati wa shibe na wakati wa njaa; wakati wa kuwa na wingi wa vitu na wakati wa kupungukiwa. 13 Naweza kufanya mambo yote katika yeye anipaye nguvu.
14 Hata hivyo, mlifanya vizuri kunisaidia kwa kushirikiana nami katika taabu zangu. 15 Ninyi ndugu zangu Wafilipi mnajua kwamba nilipoanza kuhubiri Injili, nilipokuwa natoka Makedonia, hakuna kanisa lililoshirikiana nami katika kutoa na kupokea isi pokuwa ninyi. 16 Hata nilipokuwa Thesalonike, mliniletea msaada zaidi ya mara moja. 17 Msifikiri kwamba napenda sana kupokea zawadi, sivyo. Ninachotaka kuona ni matunda ambayo kama yak iongezeka ni faida kwenu. 18 Nimekwishapokea malipo yangu yote na ziada. Sasa ninavyo vitu tele kwa sababu Epafrodita amekwisha niletea zawadi zenu. Hakika zawadi hizi ni matoleo yenye harufu nzuri ya manukato inayokubaliwa na kumpendeza Mungu. 19 Na Mungu wangu atawapeni ninyi kila kitu mnachohitaji kwa kadiri ya uta jiri wake mtukufu katika Kristo Yesu. 20 Mungu wetu na Baba yetu apewe utukufu milele na milele. Amina. 21 Natuma salamu zangu kwa kila mtu wa Mungu katika Kristo Yesu. Ndugu ninaokaa nao pia wanawasalimu. 22 Vile vile watu wote wa Mungu wa hapa na hasa wale wa nyumba ya Kaisari, nao pia wanawasalimu.
1 Kutoka kwa Paulo, mtume wa Kristo Yesu na Timotheo ndugu yetu. 2 Kwa ndugu katika Kristo, watakatifu na waaminifu waishio Kolosai. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
Shukrani Na Maombi
3 Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunapowaombea. 4 Kwa maana tumepata habari juu ya imani yenu katika Kristo Yesu na upendo wenu kwa watu wote wa Mungu. 5 Imani hii na upendo umetokana na tumaini mlilowekewa mbinguni na ambalo mmelisikia katika neno la kweli, yaani Habari Njema. 6 Duniani kote, hii Habari Njema iliyowajia inaenea na kuzaa mat unda kama ilivyokuwa kwenu mlipoisikia na kuelewa neema ya Mungu kwa kina.
7 Mlijifunza juu ya Habari Njema kutoka kwa mtumishi mwenzenu mpendwa, Epafra. Yeye ni mhudumu mwaminifu wa Kristo ambaye ana fanya kazi kwa niaba yetu, 8 naye ametufahamisha juu ya upendo wenu mliopewa na Roho.
9 Kwa sababu hii, tangu tuliposikia habari zenu, hatujaacha kuwaombea. Tunamsihi Mungu awape kwa wingi, maarifa ya kujua mapenzi yake, kwa njia ya hekima ya kiroho na ufahamu. 10 Ili mpate kuishi maisha yanayomtukuza Bwana na kumpendeza kabisa: mkizaa matunda kwa kila kazi njema na kukua katika kumjua Mungu. 11 Tunawaombea pia muimarishwe na nguvu zote kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake; mpate kuwa na subira na uvumilivu, huku 12 mkimshukuru kwa furaha Baba aliyewafanya mustahili kuwa na fungu katika urithi wa watakatifu, katika ufalme wa nuru. 13 Kwa maana ametuokoa kutoka katika nguvu za giza, akatuweka katika ufalme wa Mwanae mpendwa, 14 ambaye ametukomboa kwa damu yake, tukapata msamaha wa dhambi.
Ukuu Wa Kristo
15 Kristo anafanana kabisa na Mungu asiyeonekana. Yeye ali kuwepo kabla Mungu hajaumba kitu cho chote. 16 Yeye ndiye ali yeumba vitu vyote mbinguni na duniani; vitu vinavyoonekana na visivyoonekana; kama ni viti vya enzi au nguvu, au watawala au milki na mamlaka: vyote viliumbwa na yeye kwa ajili yake. 17 Yeye alikuwapo kabla ya vitu vingine vyote na kwa uwezo wake vitu vyote vinahusiana kwa mpango. 18 Yeye ni kichwa cha mwili, yaani kanisa lake; naye ni wa kwanza na mzaliwa wa kwanza wa wale wote wanaofufuka kutoka kwa wafu, ili yeye peke yake awe mkuu katika vitu vyote. 19 Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba ukamil ifu wake wote wa kimungu uwe ndani ya Mwanae; 20 na kwamba kwa njia ya mwanae vitu vyote vilivyoko duniani na vilivyoko mbinguni vipatanishwe na Mungu, kwa ajili ya damu yake iliyomwagwa msala bani kuleta amani.
21 Hapo kwanza ninyi mlikuwa mmefarakana na Mungu na mlikuwa maadui zake kwa sababu ya mawazo na matendo yenu maovu. 22 Lakini sasa Mungu amewapatanisha naye kwa njia ya mwili wa Kristo katika kifo, ili awaweke mbele yake mkiwa watakatifu, bila doa wala lawama. 23 Lakini hamna budi kuendelea kuwa imara na thabiti katika imani yenu, pasipo kuyumba katika tumaini lililomo katika Injili. Hii ndio ile Injili mliyoisikia na ambayo imetan gazwa kwa kila kiumbe duniani na ambayo mimi, Paulo, nimekuwa mtumishi wake.
Huduma Ya Paulo Kwa Makanisa
24 Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu na kwa mateso yangu ninakamilisha kile ambacho kimepungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, yaani kanisa lake. 25 Mimi nime kuwa mtumishi wa kanisa kufuatana na wajibu niliopewa na Mungu, kuwasilisha kwenu neno la Mungu kwa ukamilifu. 26 Hii ni siri ambayo ilikuwa imefichika kwa karne nyingi na vizazi vingi viliv yopita, lakini sasa imefunuliwa kwa watu wa Mungu. 27 Kwao, Mungu amependa kudhihirisha kati ya mataifa utukufu wa utajiri wa siri hii, yaani, Kristo ndani yenu ndiye tumaini pekee la utu kufu.
28 Kwa sababu hii tunamtangaza Kristo, tukiwaonya na kuwa fundisha watu wote kwa hekima yote ili tuweze kumleta kila mmoja mbele ya Mungu akiwa amekamilika katika Kristo. 29 Kwa shabaha hii nina fanya kazi, nikijitahidi kwa nguvu kuu ya Kristo inay ofanya kazi kwa uwezo mkuu ndani yangu.
2 Napenda mjue jinsi ninavyofanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu na kwa ajili ya watu wa Mungu walioko Laodikia, na kwa ajili ya wengine wote ambao hawajapata kuniona. 2 Shabaha yangu ni kuwa wafarijiwe moyoni na kuunganishwa katika upendo, ili wapate uta jiri wa ufahamu kamili, wajue siri ya Mungu, yaani Kristo; 3 ambaye kwake hupatikana hazina yote ya hekima na maarifa. 4 Nawaambia haya ili mtu ye yote asije akawadanganya kwa maneno ya kuvutia. 5 Maana ingawa mimi niko mbali nanyi kimwili, lakini niko pamoja nanyi kiroho, nami nafurahi mnaendelea vizuri na kwamba imani yenu katika Kristo ni imara.
Maisha Kamili Katika Kristo
6 Basi, kama mlivyompokea Kristo Yesu kuwa Bwana, endeleeni kuishi ndani yake. 7 Muwe na mizizi ndani yake, na kujengwa juu yake; mkiimarishwa katika imani kama mlivyofundishwa na kububu jika kwa shukrani.
8 Angalieni mtu ye yote asiwateke kwa falsafa duni na potofu ambazo hutegemea mapokeo ya kibinadamu na mafundisho ya kidunia, na wala si Kristo mwenyewe. 9 Maana, ukamilifu wote wa kimungu umo ndani ya Kristo katika umbile lake la kibinadamu. 10 Nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Kristo, ambaye yeye ni mkuu juu ya kila uwezo na kila mamlaka. 11 Katika Kristo mmetahiriwa kwa kuondolewa hali yenu ya asili ya dhambi. Hii si tohara inayofa nywa kwa mikono ya binadamu bali inafanywa na Kristo. 12 Mli zikwa pamoja naye katika ubatizo na kufufuliwa pamoja naye kwa kuamini uweza wa Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu.
13 Mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya dhambi zenu na kwa sababu ya kutotahiriwa kwa hali yenu ya asili ya dhambi, Mungu aliwafa nya hai pamoja na Kristo. Alitusamehe dhambi zetu zote, 14 baada ya kufuta kabisa hati ya mashtaka iliyokuwa inatukabili na kutu pinga pamoja na masharti yake; aliiondoa akaipigilia msalabani. 15 Na baada ya kuvunja nguvu na mamlaka ya shetani, Mungu alim fedhehesha hadharani kwa kuonyesha ushindi wa msalaba juu yake.
16 Kwa hiyo msimruhusu mtu awahukumu kuhusu chakula au kiny waji, au juu ya kuadhimisha sherehe za dini, sikukuu ya mwezi mpya au siku ya sabato. 17 Maana hizi zilikuwa ni kanuni za muda tu au vivuli vya yale mambo ambayo yangekuja; lakini hakika ya mambo yenyewe ni Kristo. 18 Msikubali kuhukumiwa na mtu ye yote anayejifanya mnyenyekevu na asemaye kwamba ni lazima kuabudu mal aika, mkapoteza tuzo yenu. Mtu kama huyo hufurahia kueleza kwa kirefu maono aliyoona na mawazo yake yasiyo ya kiroho humfanya awe na kiburi. 19 Mtu kama huyo amepoteza uhusiano na Kristo ambaye ni kichwa ambacho kimeunganika na mwili wote na kushika manishwa pamoja kwa mishipa yake na kukua kama Mungu apendavyo.
Kufa Na Kuishi Pamoja Na Kristo
20 Ikiwa mmekufa pamoja na Kristo na hamtawaliwi tena na kanuni za dunia hii, kwa nini bado mnaishi kana kwamba bado mna tawaliwa na masharti ya kidunia? 21 “Usishike hiki! Usionje hiki! Usiguse hiki!” 22 Masharti haya yote hayana budi kuteke tea kwa sababu yanatokana na sheria na mafundisho ya binadamu. 23 Masharti yenyewe yanaonekana kuwa ni ya hekima, maana yana jiwekea namna zake za ibada, unyenyekevu bandia na kuuadhibu mwili. Lakini hayana uwezo wo wote kuzuia tamaa za mwili.
Maisha Mapya
3 Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, elekezeni mioyo yenu kwenye mambo ya juu, alikokaa Kristo, upande wa kulia wa Mungu. 2 Yafikirini mambo ya juu na siyo mambo ya hapa duniani. 3 Kwa maana ninyi mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo kwa Mungu. 4 Wakati Kristo ambaye ni uzima wetu ataonekana, ndipo na ninyi mtakapoonekana pamoja naye katika utu kufu.
5 Basi, yaangamizeni kabisa mambo yote yanayotokana na asili yenu ya kidunia: uasherati, mawazo machafu, tamaa mbaya, nia mbaya na choyo ambayo ni ibada ya sanamu. 6 Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu ya Mungu inakuja. 7 Ninyi mlikuwa mkitenda mambo haya katika maisha yenu ya zamani. 8 Lakini sasa ni lazima mwa chane kabisa na mambo kama haya: hasira, ghadhabu, nia mbaya, matukano na maneno machafu kutoka vinywani mwenu. 9 Msiambiane uongo kwa maana mmekwisha vua utu wenu wa zamani pamoja na matendo yake 10 na kuvaa utu upya ambao unaendelea kufanywa upya katika ufahamu ili ufanane na Muumba wake. 11 Katika hali hii hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, mtu aliyesoma na asiyesoma, mtumwa na mtu huru. Bali Kristo ni yote na yumo ndani ya wote. 12 Basi, kwa kuwa ninyi ni wateule wa Mungu, wapendwa na watakatifu, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13 Vumilianeni na kusameheana kama mtu ana malalamiko kuhusu mwenzake. Sameheni kama Bwana alivyokwisha kuwasamehe. 14 Juu ya haya yote, vaeni upendo ambao unaunganisha mambo haya kuwa kitu kimoja kilicho kikamilifu.
15 Ruhusuni amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena muwe na shukrani. 16 Neno la Kristo lidumu ndani yenu kwa wingi, mki fundisha na na kuonyana katika hekima yote; na huku mkiimba zab uri, nyimbo na tenzi za rohoni na mkiwa na shukrani kwa Mungu mioyoni mwenu. 17 Na lo lote mtakalofanya, ikiwa kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.
Wajibu Katika Familia
18 Ninyi wake, watiini waume zenu kama inavyopasa katika Bwana. 19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu wala msiwe wakali juu yao. 20 Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hii humpendeza Bwana. 21 Ninyi akina baba msiwachokoze watoto wenu wasije wakakata tamaa.
22 Nanyi watumwa, watiini mabwana wenu wa hapa duniani katika mambo yote; fanyeni hivyo kwa moyo safi mkimwogopa Mungu, na wala si kwa kutafuta upendeleo wakati wanapowatazama. 23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana na siyo wanadamu. 24 Kwa maana mnafahamu kwamba mtapokea urithi wenu kwa Bwana kama tuzo yenu.
4 Ninyi mnamtumikia Bwana Kristo. Mtu atendaye uovu atalipwa kwa uovu wake, wala hakuna atakayependelewa. Ninyi mabwana, watendeeni watumwa wenu haki na ilivyo sawa mkitambua ya kwamba ninyi pia mnaye Bwana mbinguni.
Maagizo Zaidi
2 Dumuni katika maombi, mkikesha na kushukuru. 3 Pia tuom beeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango tupate kutoa ujumbe wetu na kuitangaza siri ya Kristo ambayo kwa ajili yake mimi nimefungwa gerezani. 4 Ombeni kwamba niwezeshwe kuitangaza Injili kwa ufasaha, kama inipasavyo kusema.
5 Muwe na hekima katika uhusiano wenu na watu wasioamini, mkiutumia wakati wenu vizuri. 6 Mazungumzo yenu yawe ya unyen yekevu wakati wote, yawe ya kuvutia, ili mjue jinsi ya kumjibu kila mtu.
7 Tikiko atawaelezeeni habari zangu zote. Yeye ni ndugu mpendwa, mfanyakazi mwaminifu na mtumishi mwenzangu katika Bwana. 8 Nimemtuma kwenu kwa madhumuni kwamba mpate kufahamu hali yetu na pia awatie moyo. 9 Anakuja pamoja na Onesmo ndugu yetu mpendwa na mwaminifu, ambaye ni mtu wa kwenu. Watawaelezeeni mambo yote yanayotendeka huku.
Salamu Na Maagizo Ya Mwisho
10 Aristarko aliyefungwa gerezani pamoja nami anawasalimu, hali kadhalika Marko, binamu yake Barnaba, anawasalimu. Mmek wisha kupokea maagizo yanayomhusu. Akija kwenu, mpokeeni. 11 Na Yesu, yule aitwaye Yusto, pia anawasalimuni. Hawa tu, ndio Way ahudi kati ya watu tunaofanya nao kazi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, nao wamekuwa faraja kwangu. 12 Epafra, ambaye ni mtu wa kwenu, na mtumishi wa Kristo Yesu , anawasalimu. Yeye anawaombea kwa bidii kila wakati kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mungu mkiwa mmekomaa na mkiwa thabiti. 13 Ninashuhudia kwamba anaomba kwa bidii kwa ajili yenu na kwa ajili ya ndugu wa Laodikia na Hierapoli. 14 Luka, yule daktari mpendwa, pamoja na Dema, wanawasalimu. 15 Nisalimieni ndugu wote wa Laodikia na pia Nimfa pamoja na kanisa linalokutana nyumbani kwake.
16 Mkisha somewa barua hii, hakikisheni kuwa inasomwa pia na ndugu wa Laodikia. Na ninyi pia hakikisheni kuwa mnasoma barua inayotoka Laodikia.
17 Mwambieni Arkipo hivi: “Hakikisha kuwa unakamilisha ile huduma ambayo umeipokea katika Bwana.”
Copyright © 1989 by Biblica